Ticker

7/recent/ticker-posts

KANISA LA ARISE AND SHINE NI ZAIDI YA MADHABAHU

Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa, kuongoza wa Kanisa la Arise and Shine.

 NA JIMMY KIANGO

Ni jambo la kawaida kwa siku za Jumamosi, Jumapili, Jumatatu na Jumanne kushuhudia maelfu ya watu wakifurika kwenye viwanja vya Tanganyika Pakers, vilivyopo Kawe, jijini Dar es Salaam.

 

Kama hujui lolote kuhusu Boniface Mwamposa na kanisa lake la Arise and Shine, unaweza kujiuliza hao watu wanakwenda wapi na huko wanakokwenda wanakwenda kufanya nini?

 

Jibu la swali hilo ni jepesi tu. Watu hao wanakwenda kusaka uponyaji, amani na furaha kwenye madhabahu ya Kanisa la Arise and Shine inayoongozwa na Mwamposa. 

 

Nabii na Mtume Boniface Mwamposa, maarufu kama "Bulldozer ", amejipatia umaarufu mkubwa si tu kwa sababu ya mahubiri yake yenye mvuto na nguvu za kiroho, bali pia kwa namna anavyogusa maisha ya watu katika nyanja mbalimbali. 

 

Makala hii inaangazia maeneo matano muhimu yanayoonesha mchango wa kanisa hili kwa jamii na taifa kwa ujumla.


 

NGUVU YA MAOMBI, MAOMBEZI NA UPONYAJI

Moja ya sababu kubwa zinazowavuta maelfu ya watu kuhudhuria ibada za Kanisa la Arise and Shine ni huduma ya maombi na maombezi inayoambatana na uponyaji wa miujiza. 

 

Kupitia mikutano ya maombi, watu wanaokumbwa na changamoto mbalimbalikiroho, kimwili na kiakili hujumuika kwa imani kubwa wakiamini kupata mabadiliko ya maisha.

 

Huduma hizi zimeleta matumaini kwa baadhi ya wagonjwa  waliokata tamaa hospitalini, watu waliovamiwa na mapepo au waliopitia vifungo vya kiroho.

 

Shuhuda kutoka kwa waumini waliopona magonjwa sugu au waliofunguliwa kutoka katika vifungo vya maisha ni ushahidi tosha wa nafasi ya kiroho ambayo kanisa hili linatimiza.

 

KUCHECHEMUA UCHUMI WA MTU MMOJA MMOJA

 

Wakati wa ibada kuu au mikutano mikubwa ya kiroho, maelfu ya watu humiminika Kawe au popote mikutano yake itakapokuwa kutoka pande mbalimbali za nchi.

 

Tukio hili linakuwa fursa ya kiuchumi kwa wafanyabiashara wa vyakula, vinywaji, mavazi ya kidini, pamoja na watoa huduma za usafirishaji kama bodaboda, bajaji na daladala.

 

Wachuuzi wengi wa eneo hilo wanasema kuwa kila ibada kubwa ni “sikukuu ya kipato.” Hii inaonesha namna kanisa linavyochangia katika kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja kwa vitendo, tofauti na dhana kuwa makanisa yapo tu kwa ajili ya mafundisho ya kiroho.

 


KUIBUA DIRA YA MAENDELEO KWA WAFUASI WAKE

Kupitia mafundisho ya Nabii Mwamposa, waumini wengi wamehamasishwa kuamka kiakili na kujitambua. 

 

Mchungaji huyo amekuwa akisisitiza kuhusu maisha ya ustawi, kuamka kiuchumi na kutumia vipaji vya mtu binafsi kwa ajili ya mafanikio ya dunia hii na ya mbinguni.

 

Kanisa linawahamasisha watu kuwekeza, kuanzisha biashara, kujifunza stadi mpya na kutokubali kubaki katika umasikini. 

 

Kwa njia hii, Arise and Shine limekuwa jukwaa la mabadiliko kwa watu wengi waliokuwa wamekata tamaa ya maisha.

 

KUIMARISHA MAADILI YA KIJAMII

Mbali na kuhubiri habari njema ya wokovu, Kanisa la Arise and Shine linatoa mafundisho ya kimaadili yanayolenga kujenga jamii yenye hofu ya Mungu, inayozingatia maadili na kuheshimu sheria. 

 

Kupitia mafundisho hayo, watu wengi wameacha ulevi, wizi, uzinzi na hata kuacha kushiriki katika vitendo vya rushwa.

 

Kwa muktadha huo, mchango wa kanisa hili unakwenda mbali zaidi ya kiroholinalenga kujenga taifa lenye raia waadilifu, wenye heshima na uwajibikaji. 

 

Hili ni jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa katika ustawi wa kitaifa, hasa katika kupambana na mmomonyoko wa maadili.

 


MSAADA KWA WENYE UHITAJI

 

Kanisa pia limekuwa likijihusisha na kusaidia makundi yenye uhitaji kama vile yatima, walevi waliotaka kuachana na uraibu,wafungwa pamoja na watu waliopoteza matumaini ya maisha. Wapo pia wanaotumia kusanyiko hilo kuanzisha biashara ndogondogo.

 

Kwa njia hii, Arise and Shine linatoa nafasi kwa watu waliokata tamaa kurejea katika jamii wakiwa watu wapya, wenye malengo mapya ya maisha.

 

Kanisa la Arise and Shine si mahali pa ibada tu, bali ni kitovu cha mabadiliko ya maisha ya watu kiroho, kiuchumi na kijamii. 

 

Kupitia huduma ya Nabii Boniface Mwamposa, jamii ya Kawe na Tanzania kwa ujumla imekuwa ikishuhudia athari chanya za kiimani, kiuchumi na kimaadili.

 

Katika zama ambazo taasisi nyingi za kidini zimekuwa zikilaumiwa kwa kukosa mguso wa moja kwa moja kwa jamii, Arise and Shine limekuwa mfano wa taasisi inayogusa maisha ya watu kwa undanikwa maneno na kwa vitendo.

 

 


Post a Comment

0 Comments