Ticker

7/recent/ticker-posts

VISION PLUS KINARA WA MATIBABU YA MACHO TANZANIA,ND. DATOO AMPONGEZA RAIS SAMIA

Nd. Datoo akiwa na Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.

VISION PLUS KINARA WA MATIBABU YA MACHO TANZANIA

*Nd. Datoo ampongeza Rais Dkt. Samia kwa kuitangaza nchi kimataifa

Jarida la Tz&Beyond limefanya mahojiano na Mtaalam bingwa wa macho nchini Tanzania, ambaye pia ni mmiliki wa kituo bora cha kutoa huduma za macho cha Vision Plus, Nd. Husseinali Datoo. Fuatilia mahojiano hayo.

Nd. Huseinali Datoo anajulikana kitaifa na kimataifa,amelitumikia taifa la Tanzania kwa zaidi ya miaka 40 akitoa huduma ya macho.

Mtaalamu huyu alizaliwa Tunduru mkoa wa Ruvuma, wazazi wake  waliishi huko na kufanya biashara tangu mwaka 1919.

Baada ya kumaliza masomo ya Shule ya msingi Tunduru na baadaye Sekondari Lindi  na Dar es Salaam alienda Uingereza kusomea masuala ya Optometry, alihitimu mwaka 1976 na kufanya kazi nchini humo kwa miaka miwili kwenye mji wa London. Mwaka 1978 alirudi Tanzania.

TZ & BEYOND: Wewe ni nani hasa?

ND. DATOO: Mim ni  mtaalamu wa macho (OPTOMETRIST) na kazi yangu ni kutoa huduma inayoweza kumsaidia mtu kuona.

Tunaangalia macho na kupimia  vipimo vya kuona na pia kufuatilia hali za macho (Diagnosis) zinazohusiana na matibabu na magonjwa kama vile kisukari, kudhibiti na kutibu shida ya Jicho Pevu na Glakoma na pia tunatoa miwani ya macho.

 TZ & BEYOND: Vision Plus imeanza lini?

ND. DATOO:Vision Plus awali ilijulikana kwa jina ya Medical Eye Centre  ilianzishwa mwaka 1979 tukiwa na kitengo kidogo kwenye barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1984 tulikuwa na kufungua tawi Zanzibar  na maeneo mengine.

Hapa Dar es Salaam tupo Shoppers plaza, Samora Tower na Afya House Mikocheni.

TZ & BEYOND: Kuna changamoto ya wataalamu wa macho, hapa hali ikoje?

ND. DATOO: Ni dhahiri bado hatuna wahudumu wa afya wa macho wa kutosha kusaidia mamilioni ya watu wanaougua ugonjwa huo nchini.

Hata hivyo jitihada zinaendelea, Wizara ya Afya imekuwa ikitoa mafunzo na kuwawezesha wengi zaidi kusomea fani ya macho.

Mwaka 1978 shule ya macho ilianzishwa mjini Moshi KCMC na tangu wakati huo imeanza nyingine Dodoma na Iringa hivyo naamini katika miaka ijayo Tanzania itakuwa na wataalamu wengi wa macho natumai, hapa kwetu tunajitahidi, maana tutawezesha kutoa wataalamu wa kutosha.


TZ & BEYOND: Changamoto ya vifaa tiba vya macho nayo likoje hapa Vision Plus?

ND.DATOO: Tuna vifaa vya hali ya juu vya kutambua hali ya macho na kwenda na wakati, tumewekeza katika teknolojia ya kisasa.

Tuna kamera ambayo inaweza kugundua magonjwa kama vile kisukari, glaucoma    ( shinikizo la macho).nk.

Pia tunaweka lenzi katika miwani na tunatumia mashine za kisasa.

TZ & BEYOND: Vision Plus inahudumia watu wa namna gani?

ND.DATOO: Kusema ukweli katika miaka 40 iliyopita tumejenga wateja wetu na lengo letu limekuwa kumtumikia kila mteja kutoka tabaka la chini hadi watu wa juu kabisa, itoshe kusema kwamba tunafurahia kuwahudumia viongozi wetu, wengi wamekuwa nasi tangu kuanzishwa kwetu na huduma za macho tunazotoa ni za viwango vya juu.

TZ & BEYOND: Tatizo la macho ni kubwa kisi gani nchini?

ND. DATOO: Hivi karibuni tumeona matatizo mengi ya macho  yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari pamoja na hayo katika zama za matumizi ya simu janja, kompyuta pia husababisha tatizo la uoni hafifu kuongezeka nchini Tanzania.             Hivyo nikiri, tatizo ni endelevu sana na lina athiri kuona.

TZ & BEYOND: Mna mpango wa kufungua matawi zaidi?

ND. DATOO: Ndio, kama nilivyosema awali, tunayo matawi Dar es Salaam, lakini pia tunafikiria kufungua tawi Dodoma.

TZ & BEYOND: Hapa gharama za matibabu zikoje?

ND. DATOO: Ni kweli gharama za matibabu ya macho ni kubwa, lakini pia inategemea na tatizo linalomkabili mgonjwa.

Kwetu gharama ni za kawaida, siwezi kusema ni kubwa au ni ndogo, tunajitahidi huduma iwe kwa bei nafuu na bora.

TZ & BEYOND: Kipi ni kisababishi  cha matatizo ya macho?

ND. DATOO: Viwango vya maambukizi ya upofu vinatofautiana sana lakini ushahidi unaonyesha kuwa upofu unazidi Afrika na Tanzania pia.

Chanzo kikuu ni pamoja na ujio wa kompyuta na simu na macho kupata uchovu kwa urahisi na kusababisha matatizo.

Hali nne za kawaida za macho zinazosababisha kupoteza uwezo wa kuona au upofu ni: Mtoto wa jicho (Cataract) Retinopathy inayohusiana na ugonjwa wa sukari. Glakoma.(shinikizo la damu la macho) na upungufu wa lishe (Vitamins) kwa watoto wachanga.

TZ & BEYOND: Nini kifanyike kulinda afya ya macho?

ND. DATOO: Kuna magonjwa mbalimbali ya macho na matatizo ya kuona. Baadhi yake hayana tiba, lakini mengine mengi yanaweza kutibika. Unaweza kujiepusha kwa kufuata mtindo mzuri wa maisha na kuangalia afya ya macho mara kwa mara na chakula chenye lishe haswa kwa  watoto.


TZ & BEYOND: Ushirikiano wa Vison Plus na Serikali ukoje?

ND. DATOO: Mimi binafsi, nimejihusisha na chama chetu cha wataalamu wa macho Tanzania Optometric Association (TOA) kwa miaka 25 sasa, nilikuwa sehemu ya mchakato wa juu wa kuhamasisha wadau kuanzisha Optometry ACT 2017 Bungeni  ambapo Optometry ilitambulika kama taaluma nchini Tanzania.

Pia Vision plus ilikuwa mstari wa mbele kuandaa semina kwa madaktari wa macho kila mwaka.

Pia nimekuwa katika bodi ya Baraza la Optometria, niliteuliwa na Waziri ya Afya. 

Tunahakikisha kwamba Optometrists wanadhibitiwa kama taaluma zingine hapa Tanzania na ulimwenguni.

TZ & BEYOND: Ushiriki wa Vision Plus kwa jamii, ukoje?

ND. DATOO: Tunaamini katika kurudisha kwa jamii yetu na uwajibikaji wa kijamii ndio dhamana kuu ambayo tumehusika nayo na nI wajibu wetu pia!

Tumekuwa tukifanya hivyo tangu mwaka 1984 na tumekuwa tukipanga kambi za macho kusaidia wasiojiweza.

Kambi ya macho ya kwanza ilikuwa Bagamoyo mwaka 1982  na baadaye Zanzibar mnamo mwaka 1985. Kambi za macho zimekuwa zikiendelea na hadi leo tunafanya hivyo.

Hapo Tunduru nilipozaliwa tulikuwa na kambi kubwa ya macho mwaka 2016  kwa kushirikiana na Bilal na tulihudumia watu wengi na ilinipa furaha kuwahudumia watu wa Tunduru na pia tutaendelea na jitihada hizo.

TZ & BEYOND: Matamanio yako ni yapi kwenye kukabiliana na tatizo la macho nchini?

ND. DATOO: Natamani kupanua zaidi uwajibikaji wetu wa kijamii wa shirika katika vijiji ambako kunahitajika huduma ya macho zaidi ili watu wapate huduma za macho kwa bei nafuu.


TZ & BEYOND:Upi ujumbe wako kwa Serikali?

ND.DATOO: Kwanza nampongeza Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania duniani na pia kwa uongozi wake makini.

Mimi binafsi naamini kuishi kama raia mwema na kwa uwaminifu wa nchi yetu Tanzania na kufanya kitu ambacho kinachangia ustawi wa taifa letu, kuishi maisha yenye usawa na kutumia kanuni za kimaadili katika fani yangu (Optometry) na pia  kusaidia wananchi wenzangu katika huduma ya macho kwa moyo na uaminifu.

Hatimaye tunawajibika kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo yetu.

  

Post a Comment

0 Comments