Ticker

7/recent/ticker-posts

DKT. MWIGULU 'ATAFUTA' SULUHU YA UHABA WA DOLA NCHINI

Uhaba wa Dola ya Marekani kwenye mzunguko wa fedha nchini umemuibua Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambae ameiona haja ya  kuwaagiza watalaamu wa Wizara yake na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kujadili namna ya kushughulikia changamoto hiyo.

Dhamira ya kufanya hivyo ni kukabiliana na  athari za upungufu wa dola za Kimarekani katika mzunguko wa fedha ili kunusuru uchumi wa Nchi zinazoendelea.

Dkt. Nchemba, ametoa maagizo hayo wakati wa kufungua kikao kilichowashirikisha Wataalamu kutoka Shirika la Fedha na Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya Program ya Huduma za Mikopo (EFC), kwa kushirikiana na Wataalamu wa ndani wa Serikali.


Amesema mabadiliko ya Sera za Fedha nchini Marekani ya kubana matumzi na kupunguza dola kwenye mzunguko wa fedha, yameleta athari zinazoonekana mpaka kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania.

“Tumekuwa tukirejea Covid 19 na vita baina ya Urusi na Ukraine kama moja ya vitu vinavyoathiri uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania lakini upungufu wa dola unaathiri uchumi kwa kiwango kikubwa ikiwemo uagizaji wa mafuta na uagizwaji wa bidhaa mbalimbali zinazotumika katika shughuli za Sekta binafsi”. amesema

Post a Comment

0 Comments