Ticker

7/recent/ticker-posts

NDEGE YA MIZIGO YAWASILI, RUBANI MWANAMKE APEWA DHAMANA YA KUILETA NCHINI

Mwanadada Mtanzania Neema Swai ndie amepewa dhamana ya kuweka historia ya kuwa rubani wa kwanza wa kurusha ndege kubwa ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania.

Neema anairusha ndege hiyo mpya ya mizigo (Air Tanzania Cargo) Boeing 767-300F kutoka nchini Marekani hadi Tanzania.

Ndege hiyo itapokelewa leo nchini Tanzania kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, uliopo jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ndege hiyo inatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa nchi kuwa na uwezo wa kisafirisha mizigo yake haraka kwenye vituo vya kikanda na vya kimataifa.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba zaidi ya tani 50 za mizigo na inaweza kukaa angani kwa saa 10.


Post a Comment

0 Comments