Ticker

7/recent/ticker-posts

NGUVA SI SAMAKI MTU NI NG’OMBE BAHARI ALIYE KATIKA HATARI YA KUTOWEKA

Picha namsa hii Indio iliyobeba simulizi la kusadikika kuwa samaki nguva ndio yuko hivyo, jambo ambulo si la kweli. 


 NA JIMMY KIANGO

Moja ya simulizi la kusadikika liliyovishwa uhalisia kwa miaka mingi ni lile la samaki jamii ya nguvu kudaiwa kuwa eti! nusu ni Samaki na nusu mwanamke mrembo mwenye hipsi za haja. Hii sio kweli.


Simulizi hili limekuwa likisimuliwa na watu wazima mbele ya watoto wao, aidha kumekuwa na machapisho, tamthilia na vikatubi kadhaa yanayohalalisha suala hilo la kusadikika.


Sasa ukweli wa nguva ni huu, kihistoria, simulizi mbalimbali kutoka kwa wavuvi na wasafiri wa baharini walikuwa wakisema kuwa waliona "samaki mtu", hasa wakiwa mbali baharini. 

Inaaminika kwamba walikuwa wakichanganya nguva na viumbe vya kufikirika kama "mermaids" kutokana na umbo lake la kipekee na tabia ya kunyonyesha. 


Lakini kwa uhalisia wa kisayansi, nguva si samaki mtu, bali ni mamalia wa baharini wa kipekee anayehitaji kulindwakutokana na jamii hiyo kukuwa kwenye tishio la kutoweka.


Nguva ni mnyama wa ajabu wa baharini anayeonyesha uzuri wa asili na uwiano wa mfumo wa ikolojia ya majini. Kupotea kwake ni hasara kubwa si tu kwa mazingira bali pia kwa urithi wa kiikolojia wa Tanzania na dunia kwa ujumla, moja ya mambo tunayopaswa kuyafanya ni kuimarisha juhudi za uhifadhi kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Picha hii inabeba uhalisia wa nguva ndani ya bahari akiwa anakula nyasi bahari.
Nguva ni samaki wa namna gani?

Nguva, anayefahamika kitaalamu kama Dugong dugon, si samaki halisi bali ni mamalia wa majini kama vile nyangumi na pomboo. 


Ingawa huitwa "samaki mtu" kutokana na umbo lake na tabia zake zinazofanana na binadamu (kama kunyonyesha na kupumua kwa mapafu), nguva si miongoni mwa samaki wa kawaida wanaopumua kwa mabuu bali ni mamalia kamili. 


Ana mwili mkubwa, mviringo kama wa tembo wa baharini, na mkia mpana unaofanana na ule wa pomboo.

Anakula vyakula gani?
Nguva ni ml
mimea (herbivore) wa baharini. Hula majani ya baharini (seagrasses), akitumia midomo yake iliyojipinda chini ambayo inamsaidia kuparua mimea hiyo kwenye sakafu ya bahari. 


Ana uwezo wa kula hadi kilo 40 za majani ya baharini kwa siku, na hutumia muda mwingi wa mchana na usiku kula.


Anaishi kwa miaka mingapi?
Nguva anaweza kuishi kwa muda mrefu, wastani wa miaka 50 hadi 70. Kuna baadhi ya ripoti zinazoonesha kwamba 
nguva mmoja anaweza kufikia hadi umri wa miaka 73 pale anapokuwa katika mazingira salama na yasiyo na vitishokwake.



Idadi yao.

Idadi halisi ya nguva nchini inakadiriwa kufikia 100 na inaelezwa amewahi kuonekana katika maeneo ya Rufiji, Mafia, Kilwa, na Zanzibar.


Ripoti za Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Uasilia (IUCN) zinaonesha kuwa nguva ni viumbe wachache mno waliobaki katika pwani ya Tanzania.

 

Hali hiyo inbafanya idadi ya nguva kwa Afrika Mashariki kuwa  ndogo sana, ikilinganishwa na maeneo mingine duniani. Hali yao ni ya kutia wasiwasi hasa kwa ukanda wa Bahari ya Hindi.


Uchache wao unafanya kadirio la kidunia kuonesha kuwa kuna takribani nguva 100,000 waliobaki, wengi wakiwa katika Ghuba ya Uajemi, Australia Kaskazini na Asia ya Kusini Mashariki.


Hata hivyo, idadi hii inapungua kutokana na uvuvi haramu, uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa makazi yao ya majani baharini.


Ni viumbe vilivyopo kwenye hatari ya kutoweka duniani
Nguva wameorodheshwa na IUCN kama viumbe walio katika hatari ya kutoweka (vulnerable species). Sababu kuu zinazoathiri uwepo wao ni
 uharibifu wa makazi yao hasa majani ya baharini.

Kuwindwa kwa ajili ya nyama na mafuta, kukwama kwenye nyavu za uvuvi na uchafuzi wa bahari.



Nini kifanyike kumlinda?
Ili kuhakikisha kuwa 
nguva wanaendelea kuwepo, uhifadhi wa makazi yao unahitajika kwa kuhakikisha majani ya baharini yanahifadhiwa na kuepuka yasiharibiwe na shughuli za binadamu.


Elimu kwa jamii inatakiwa, wananchi wa maeneo ya pwani wanapaswa kuhamasishwa na kuelezwa kuhusu umuhimu wa nguva katika mfumo wa bahari.


Aidha ipo haja kwa serikali, taasisi zake na wadau wa bahari kama ilivyo kwa IUCN kufanya ufuatiliaji na utafiti kuweka rekodi na kuimarisha sheria za ulinzi.


Kuna umuhimu wa kuendeleza mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwani nyavu haramu na uvuvi usiodhibitiwa unaathiri sana maisha ya nguva, hivyo udhibiti mkubwa unahitajika.

 

 

Post a Comment

0 Comments