| Mjumbe wa kikundi hicho Tima Zahariu |
NA JIMMY KIANGO
Moja ya changamoto zinazotesa ndoa nyingi ni uwezo wa wanandoa kufikishana kileleni.
Hatua hiyo imewafanya akina mama wa kijiji cha Moa, kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga kusaka suluhu ya changamoto hiyo kwa kuzalisha unga wa samaki na dagaa.
Unga huo ambao una mchanganyiko wa bidhaa za bahari kama Mwani, unatumika kutengeneza uji, ugali, biskuti na donati.
Akiongea uwezo wa unga huo na bidhaa zake, Katibu wa kikundi cha Fahari ya Pwani, Bi.Mwanamondo Adam alisema unga wanaoutengeneza umekuwa na matokeo chanya kwa watumiaji wa jinsia zote.
"Tumeanza kazi ya utengenezaji Oktoba 2024, na tumekuwa tukiwauzia watu wa jinsia zote, na wanaotumia wamekuwa wateja wetu wa kudumu." Amesema.
Hata hivyo kiongozi huyo wa kukundi amesema pamoja na ubora wa bidhaa zao, lakini soko bado ni changamoto kwao.
Kwa upande wake mjumbe wa kikundi hicho Tima Zahariu amesema pamoja na kukabiliwa na ugumu wa soko, bado hawajaacha kuzalisha bidhaa zao kwa sababu wanaamini iko siku soko litafunguka kwa sababu kitu wanachokifanya ni bora na pamoja na kuimarisha ndoa, lakini pia kina faida kubwa kwa mwili wa binadamu.
Tima alisema wana uwezo wa kuzalisha kwa pakti 30 za biskuti, donati na vikokoto kwa siku, huku wakizalisha zaidi ya kilo 50 za unga wa samaki na unga wa dagaa.
Kikundi hicho kinaundwa na wakina mama 11, ambao wote wanaishi kwenye kijiji cha Moa.
0 Comments