Ticker

7/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA MBEYA WAASWA KUTOSHIRIKI MGOMO WOWOTE ULE

 

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania kwa Mkoa wa Mbeya Charles Sionga.

NA MWANDISHI WETU-MBEYA

Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanaofanyabiashara zao mkoani  Mbeya wameaswa kutotekeleza agizo la mgomo linalo sambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Wametakiwa kutofanya hivyo kwa kuwa tangazo hilo linalohamasisha mgomo kwa wafanyabiashara halipo kisheria.  

 Aliyetoa ombi hilo kwa wafanyabiashara wa Mbeya ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania kwa Mkoa wa Mbeya Charles Sionga.

 

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya Habari mkoani hapa baada ya kuona taarifa za mgomo wa Wafanyabiashara zisizo halali zikisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Sionga alisema haioni tija ya mgomo huo kwani mara zote serikali imekuwa sikivu na imekuwa ikisikiliza maombi yao kwa njia ya mazungumzo na si mgomo.

" Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania, hatujatoa tangazo lolote la mgomo huu, usio na kikomo isipokuwa nasi tunashangaa kuona taarifa zikisambaa kwenye  Instagram, Facebook, pamoja na  group za WhatsApp." Alisema Sionga.

 

Amesema, tangazo hilo limeainisha  Mikoa ya Mbeya, Iringa, Mwanza, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa na wale wa maeneo mengine kuwa wanapaswa kufunga biashara zao kuanzia kesho Juni 25, 26, 2024 bila ukomo na kwamba kutakuwa na kikosi kazi kitakacho simamia zoezi hilo. 

 

"Wafanyabiashara tunafahamu taratibu na miongozo ya kudai haki kama malalamiko ya uwepo wa kodi kandamizi yanashughulikiwa na uongozi na tayari baadhi ya viongozi wanatarajia kukutana na mamlaka za serikali,”alisema.

 

Post a Comment

0 Comments