TANGAZO KWA UMMA
Kampuni ya TANJA imeandaa mradi wa nishati safi ya kupikia katika wilaya ya Karatu unaoitwa “Mpango wa majiko sanifu ndani ya wilaya ya Karatu, Tanzania”
Malengo ya mradi huu ni kuboresha maisha ya wanajamii na pia kulinda mazingira ndani ya Tanzania kwa kusambaza majiko sanifu na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa ambao hutokana na matumizi ya kuni majumbani.
Mradi huu ni kazi ambayo ipo chini ya TANJA kwa kufuata miongozo ya social carbon standards
Mradi unakusudiwa kuchukua wigo wa kaya 5000 ndani ya kata za Oldeani, Daa, Qurus, Endabashi, Endamarariek na Ganako ndani ya wilaya ya Karatu, mkoa wa Arusha.
TANJA inawakaribisha wahisani kuleta maoni na mrejesho kupitia mjumuiko wa wahisani ili kukusanya mapendekezo mkutano huo utafanyika wilaya ya Karatu ukumbi wa SUMAWE HALL uliopo Sumawe Complex Mzizizma street, tarehe 26th July 2024 kwanzia saa tatu na nusu(09:30am) mpaka saa tisa kamili(03:00pm).
Watu watakaovutiwa kujumuika basi piga namba zilizopo hapo chini
Wale watakaowiwa kutuma maoni au kuuliza taarifa zaidi kuhusu huu mradi basi wanaweza kuwasiliana na TANJA kwa barua pepe tanja.cc.project@gmail.com au kupiga namba zifuatazo 0760 957 366
0 Comments