Ticker

7/recent/ticker-posts

BENKI YA ACCESS KUWAONDOLEA WANAWAKE KERO YA MIKOPO KAUSHA DAMU MBEYA

 

Meneja Msaidizi wa Benki ya Access, Tawi la Mbeya, Daniel Masonze akitoa ufafanuzi wa mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo kwa wajasiriamali wanawake. 

 NA PENDO FUNDISHA-AFRINEWSSWAHILI-MBEYA

 Mikopo yenye mashariti magumu na riba kubwa inayotolewa bila utaratibu mitaani maarufu kama Kausha damu, imetajwa kuwa mwiba kwa maendeleo na ndoa za baadhi  ya wanawake mkoani Mbeya.

 

Baadhi ya wanawake waliozungumza na AFRINEWSSWAHILI mkoani hapa kwenye sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya Wajasiriamali yaliyoandaliwa na  Benki ya Access Tawi la Mbeya, wameipongeza serikali kwa kuendelea kuzipigia kelele taasisi kubwa za kibenki kupunguza masharti ya dhamana ambayo yamekuwa mwiba kwa wajasiriamali wadogo.

 

Wamesema, mashariti yaliyopo kwenye taasisi kubwa za fedha yanawafanya kuangukia kwenye mikopo ya kausha damu hali inayorejesha nyuma jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.

 

Mbali ya kudumaa kiuchumi, lakini pia wamaedai kuwa wamekuwa wakikimbiwa na wenza wao kutokana na kukwepa ulipaji wa madeni hayo ya makopo na kujikuta wakiachiwa jukumu la kulea watoto.

 

Mjasiriamali,Sophia Msolla akielezea ubora wa moja ya bidhaa zake zilizosindikwa kwee maonesho ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na benki ya Access Tawi la Mbeya.

"Leo hii tumefahamu, kumbe benki ya Access inatoa mikopo kwa wajasiriamali kuanzia shilingi 500,000 tena kwa riba nafuu na dhamana yake ni ya kawaida, lakini hapo awali hatukua tukilijua hili, tunahitaji elimu zaidi ya masuala ya mikopo ili kuepukana na mikopo ta kausha damu," alisesema mjasiriamali Asha Hassan.

 

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Benki ya Access Tawi la Mbeya, Daniel Masonze, amewataka wajasiriamali hususani wanawake kuhakikisha wanapata elimu ya kutosha ya mikopo hasa kwenye taasisi kubwa za  benki ili kuondokana na adha hiyo ya mikopo ya kausha damu.

 

"Katika kuhakikisha tunaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,  Access Benki imekuja na mkakati wa kutoa kipaumbele kwa  wajasiriamali wadogo hasa wanawake ambao wana nafasi ya kukopa kiasi cha shilingi 500,000 kwa riba ndogo na dhamana yake ni sawa na ile ya mitaani.

 

“Lengo letu ni kuwaondoa kwenye kitanzi cha mikopo isiyofuata utaratibu ambayo wenyewe wanaiita kausha damu,” alisema Masonze.

 

 

Post a Comment

0 Comments