Ticker

7/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI, DCPC WASHIRIKIANA KWENYE MICHEZO

 

Kikosi cha DCPC ambeo ndio mabingwa wa bonanza hilo kwa upande wa soka kikiwa na baadhi ya maofisa wa jeshi la Polisi moka wa Kipolisi Temeke.

Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam DCPC na Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke wamefanikisha adhma ya ushirikiano kwa kuanza na bonanza la michezo lililofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam. 

 

Bonanza hilo limebeba michezo zaidi ya mitano ambayo ni kukimbia na gunia, kukimbiza kuku, kuvuta kamba na burudani za muziki sambamba na nyimbo maalum kutoka kwa Polisi na Wanahabari. 

 

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda  amefungua bonanza hilo na kusema, “ni jambo jema kuona jeshi la Polisi linaendelea kuwa na ushirikiano na wanahabari sambamba na wadau mbalimbali katika shughuli za kijamii” amesema Mapunda, pia amewasisitiza kuendelea kushirikiana na makundi mbalimbali ili jamii izidi kujenga taswira nzuri kwao.

 

Aidha, Bonanza hilo limefanyika kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili ambalo limetokana na midahalo ya ulinzi na usalama inayoendelea chini ya usimamizi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kusaidia Vyombo vya Habari (IMS) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Switzerland (SDC).

Katika mchezo wa mpira wa miguu DCPC imeibuka mshindi na kuchukua vikombe vitatu likiwemo la mchezaji bora na mfungaji bora, na Jeshi la Polisi wamenyakua vikombe vya mpira wa pete na mfungaji bora.

Mwenyekiti wa DCPC, Samson Kamalamo, kulia akishiriki kukabidhi kombe la ushindi kwa Nahodha wa time ya soka ya DCPC.


Post a Comment

0 Comments