Ticker

7/recent/ticker-posts

BENKI YA EXIM YAFADHILI BONANZA LA DCPC, POLISI TEMEKE


 NA ENDREW CHALE-AFRINEWSSWAHILI-DAR ES SALAAM

 Benki ya Exim imepongeza juhudi za pamoja baina ya Wanahabari na Jeshi la Polisi nchini hasa katika mashirikiano ya kijamii ikiwemo michezo.

 

Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Benki ya Exim, Chrispin Mwakibibi wakati wa Bonanza lililoenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayosheherekewa Machi 8 ya kila mwaka.

 

Mwakibibi amebainisha kuwa, benki ya Exim imefadhili kwa heshima Bonanza hilo maalum la Polisi na DCPC lililolenga kusherehekea jitihada za kipekee zilizofanywa na wanawake katika jamii kwa ishara ya kutambua mchango muhimu uliofanywa na wanawake, pamoja na jukumu la kuendeleza na kutetea haki za wanawake hapa Tanzania.

 

"Tunajivunia kuwa pamoja na wanawake katika jamii yetu na kuonyesha msaada wetu kwa kazi yao ngumu na kujitoa kwao.

 

Matukio kama Bonanza la Polisi si tu yanasherehekea mafanikio ya wanawake bali pia yanatukumbusha umuhimu wa kusimama kwa ajili ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake." Amesema Mwakabibi

 

Ameongeza kuwa; Jitihada ya pamoja kati ya Benki ya Exim na idara ya Polisi inaonyesha umuhimu wa kutambua na kuwainua wanawake katika jamii Kupitia mipango kama Bonanza hilo, ambalo linaweza kuvutia vizazi vijavyo na kujenga mazingira yenye uwezeshaji na yenye kuunga mkono wanawake kufanikiwa.

 

‘’Huku tukitafakari mafanikio na maendeleo yaliyofanywa na wanawake hapa Tanzania, tujiunge tena katika kukuza usawa wa kijinsia, kusherehekea tofauti na kusimama kwa ajili ya haki za wanawake wote.


Pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye kujumuisha na yenye usawa ambapo kila mwanamke ana fursa ya kufanikiwa na kuleta mabadiliko.’’ Amemalizia Mwakabibi.

Aidha, katika Bonanza hilo Club ya Waandishi  DCPC iliweza kuibuka mshindi wa kwa kunyakua kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa kuwafunga Polisi Kombaini ama Polisi Jamii.

 

DCPC ilinyakuwa ubingwa huo, baada ya kuwafunga Polisi Jamii kwa mikwaju ya penalti 4-3, katika mchezo wa fainali uliokuwa wa vute nikuvute kutokana na timu zote kuoneshana umwamba ndani ya dakika 90 na kutoka suluhu bila ya kufungana.

 

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ACP. Kungu Malulu amewataka waandishi wa habari pamoja na Polisi wawe na mahusiano mazuri yenye kuleta tija katika kazi zao.

 

Nae Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), Samson Kamalamo ameipongeza timu DCPC FC kwa kuiheshimisha taaluma ya uandishi wa habari kupitia michezo.


Lakini, pia amelipongeza jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri katika kuandaa bonaza hilo ambalo limeleta tija kubwa katika kada hizo mbili ambazo mara nyingi zimekuwa zikishirikiana katika utendaji wa kazi.

Lengo la bonanza hilo lilikuwa kujenga mahusiano mazuri baina ya waandishi wa habari na jeshi la Polisi nchini.



Post a Comment

0 Comments