NA ANDREW CHALE-AFRINEWSSWAHILI- DAR ES SALAAM.
SHIRIKA la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ), limekutana na wadau wa sekta ya Afya kujadili changamoto na mafanikio katika kongamano la kutathimini program ya BACKUP Health iliyokuwa ya miaka mitatu ikiangazia sekta ya Afya nchini.
Programu hiyo ya miaka mitatu imekuwa ikifadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia FCDO ( Foreign commonwealth and Development Office ) na kutekelezwa na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika hilo la GIZ ambapo wawakilishi kutoka Serikali ya Tanzania, Ubalozi wa Ujerumani, na Ubalozi wa Uingereza na taasisi binafsi zimeweza kutoa moni yao.
Awali Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyefungua kongamano hilo, Dkt. John Jingu amepongeza mradi huo wa BACKUP Health ulio gharimu kiasi cha Euro milioni tatu, ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi huu wa Machi, 2024.
‘’Mradi huu wa BACKUP Health umekuwa muafaka na mafanikio hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika mfumo wa bima ya Afya kwa wote.
Lakini pia tumeweza kujiimarisha kwenye mifumo ya Kidijitali katika afya na hata pia kugundua baadhi ya changamoto ambazo zipo na kuweza kuzifanyia kazi ili kuhakikisha watanzania wanapatata huduma za afya wanazozistahili sehemu yoyote walipo bila kikwazo chochote ikiwemo kikwazo cha fedha.’’ Amesema Dkt. John Jingu.
Aidha, amesema kuwa magonjwa hayapigi hodi, hivyo chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya.
‘’Tukiwa na mifumo imara ndani ya nchi yetu, itamsaidia mtanzania yoyote hata yule ambaye hana pesa, atapata huduma ya afya, yaani mtanzania yoyote kupata huduma ya afya bila kikwazo chochote, haya yote yanaimarishwa.”
Kwa upande wake, Kiongozi wa Programu kutoka (German Cooperation-GIZ)-BACKUP Health, Bw. Huzeifa Bodal amebainisha kuwa, Ujerumani inaendelea katika mashirikiano ya kuboresha mifumo ya afya na Tanzania, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kufanikisha malengo sekta ya Afya.
Ameeleza kuwa, programu hiyo imesaidia kuboresha ufanisi wa huduma za afya, kushirikiana na jamii, na kuongeza ushirikiano kati ya serikali na vituo vya afya.
Nae Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani, Dkt. Katrin Bornemann amebainisha kuwa, Ujerumani itaendelea kusaidia maendeleo ya Tanzania, hususan katika sekta ya afya kwa kutoa msaada wa kiufundi na kifedha.
Hafla hii imekuwa jukwaa muhimu la kujadili mafanikio na changamoto za programu ya Backup ya Afya nchini Tanzania. Ushirikiano wa kimataifa na azma ya serikali ya Tanzania zinaashiria matumaini ya kuendelea kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii ya Kitanzania.
Washiriki kutoka Wizara ya Afya Tanzania bara na Zanzibar, lakini kutoka Asasi za kiraia,
Wengine ni wawawkilishi kutoka TNCM na ZGFCCM.
0 Comments