Ticker

7/recent/ticker-posts

WANAWAKE JIUNGENI KWENYE TEKNOLOJIA KUONGEZA UZALISHAJI MASOKO- DKT. GWAJIMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima 

 NA ANDREW CHALE-AFRINEWSSWAHILI- DAR ES SALAAM.

 Wanawake na Wasichana wametakiwa kuchangamkia fursa ya teknolojia ili kuongeza uzalishaji kwenye masoko nchini kwa kukuza uchumi, ubunifu, na kuboresha maendeleo ya jamii.

 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Mkutano wa pili wa Wanawake na Teknolojia wa Tanzania uliandaliwa na Taasisi ya The Launch Pad Tanzania (LP Tanzania), uliofanyika katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar Es salaam (UDSM) ambapo amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa, Teknolojia ni chombo muhimu katika kukuza uchumi, ubunifu, na kuboresha maendeleo ya jamii ambapo Tanzania, kama nchi nyingine duniani, inashuhudia mapinduzi ya kidijitali yanayotoa fursa ya Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na inasisitiza kutumia teknolojia na kukuza maendeleo jumuishi.

 

Amewataka washiriki kutumia kikamilifu fursa ya Mkutano huo katika kujikwamua kiuchumi na kumiliki njia kuu za uchumi kwani ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi kidigitali husaidia kwa sehemu kubwa kuondokana na ukatili wa aina zote.

 

“Kwa kutumia kauli mbiu ya siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu ya kuwekeza kwa wanawake :Kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii,tujenge msukumo katika kuwekeza kwa wanawake na wasichana katika teknolojia ili kuwa na kuongeza uzalishaji na masoko” amesema Waziri Dkt. Gwajima.

 


Aidha, Waziri Dkt. Gwajima amesisitiza maazimo ya Mkutano huo yawe ni kuongeza ufahamu, kuwa na ufumbuzi unaotokana na data, kuwawezesha wanawake katika teknolojia au wale wanaotamani kufanya kazi katika teknolojia na kuhamasisha ushirikishwaji huku njia wazi za kuwezesha na kukuza kazi zao katika tasnia ya teknolojia zikizingatiwa katika kiwasilisha miradi ya ubunifu na bidhaa za kijiditaji zilizoundwa na wanawake.

 

Aidha, katika tukio hili pia Dkt. Gwajima aliweza kukabidhi tuzo kwa Wanawake wenye mchango kwenye sekta ya teknolojia katika nyanja mbalimbali.

 

 Tuzo zilikabidhiwa kwa; Lilian Madeje (Biashara), Maria Theresa Kadushi (Afya), Rose Funja (Kilimo), Dkt. Mboni Kibelloj (Elimu), Abella Bateyunga (Teknolojia ya kidijitali) na Mhandisi Clarence Ichwekeleza (Tuzo ya Heshima).

 

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa LP Tanzania, Carlo Ndosi amemshukuru Waziri Dkt. Gwajima kwa kuungana na Wanawake wengine katika kongamano hilo huku pia akiwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo washiriki.

 

Nae Meneja wa mradi wa SHE TEC, Bi. Jacky Msambila wa LP Tanzania, kongamano hilo limekuwa la mafaniko msimu huu wa pili kwani shuguli na washiriki ziliongezeka.

“Wanawake wa tasnia ya teknolojia, wamekusanyika kujadili masuala yanayohusu uchumi wa kidigitali, kwa kutambua mchango wa Wanawake na digitali, tumetoa tuzo kwenye elimu, afya, biashara , na mifumo ya fedha inayotumia teknolojia mfano njia za malipo za kidigiti’’ amesema Jacky Msambila

 

Aidha, ametoa wito kwa Wadau kuendelea kuwekeza kwa wanawake wajikwamue kiuchumi kwa kupitia teknolojia , kwa maana wengi wanamawazo ya kibunifu, ila wanakosa msaada na sapot ya kifedha , hali na mali.

 

Post a Comment

0 Comments