Ticker

7/recent/ticker-posts

TANROADS YATAKIWA KUWANYIMA KAZI MAKANDARADI WAZEMBE

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuanzia sasa kutowapa kazi wakandarasi wote wanaochelewesha miradi ya ujenzi na menejimenti zao kuhakikisha wanaripoti ofisini kwake mara moja kwa hatua zaidi.

Amewataka wasimamizi wa miradi ya barabara  kuwa wabunifu na kusimamia majukumu yao kikamilifu ili kuondoa  changamoto kwa watumiaji wa miundombinu ya ujenzi wa barabara nchini.

Bashungwa amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua athari za mvua, mradi wa mabasi yaendayo kasi awamu ya tatu na miradi mingine ya ujenzi inayoendelea.


Amewaagiza TANROADS kuanzia sasa mradi wowote wa barabara unaojengwa nchini katika hatua ya usanifu lazima  washirikiane na taasisi zingine za Serikali ili kuondoa matatizo ya kiutendaji pale ambapo mradi unakamilika na taasisi nyingine inataka kutekeleza mradi wake eneo hilo.

Amesema atakuwa mkali kwa watendaji au wakandarasi wazembe wanaoshindwa kwenda na kasi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kusababisha miradi kusuasua.

Bashungwa ameonya tabia ya baadhi ya wakandarasi kujilimbikizia miradi mingi kwa wakati mmoja na yote kutotekelezwa kwa kasi inayotakiwa kimkataba.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Dorothy Mtenga amesema  ujenzi wa BRT III unaotekelezwa na mkandarasi  Sinohydro unatarajia kukamilila Machi 2024

Post a Comment

0 Comments