WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa ameupongeza uongozi wa Soko la Kariakoo kwa usimamizi mzuri wanaoufanya wakati wote wa ukarabati wa soko hilo.
Waziri Mchengerwa pia amempongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo mama Hawa Ghasia kwa kuongoza zoezi la usimamizi wa ukarabati.
"Leo tumefanya ukaguzi na nimeridhika kwamba, ujenzi unakwenda vizuri na takribani asilimia 85 imekwishatekelezwa.
“Lakini, pia nimpongeze Mkuu wa Mkoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, kwa usimamizi mzuri wa soko hili ambalo ndiyo kitovu cha Dar es Salaam na unapoizungumzia Dar es Salaam, unaizungumzia Kariakoo na Soko la Kariakoo lina historia kubwa sana"
Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa Jengo la Soko Kuu la Kariakoo.
0 Comments