Ticker

7/recent/ticker-posts

MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE WAPITA

Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama zaidi ya mara mbili bungeni, jijini Dodoma.

Leo Novemba 1,2023 baadhi ya Mawaziri na Wabunge walimpongeza Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Godwin Mollel.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama  na akiuridhia atausaini ili uwe Sheria.


Akiusoma bungeni Waziri Ummy amesema kuwa wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha wamependekeza baadhi ya vyanzo vya mapato vya kuendesha mfuko maalum kwa ajili ya kugharamikia matibabu ya wasiojiweza na magonjwa sugu na ya muda mrefu.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Novemba 1, wakati wa kikao cha Bunge Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote wa mwaka 2022.

Ametaja baadhi ya vyanzo vitakavyotumiwa kwa ajili ya kugharamikia mfuko huo ni pamoja na ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, kodi ya michezo ya kubahatisha, ushuru wa miamala ya kielektroniki pamoja na vyanzo vingine pendekezwa.

Pia ameongeza kuwa fedha nyingine za kuwezesha mfuko huo ni pamoja na misaada na fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.



Post a Comment

0 Comments