Ticker

7/recent/ticker-posts

MNYUKANO WA MWIGULU NA MPINA NDANI YA BUNGE WACHUKUE SURA MPYA

MPINA HAJUI HESABU, ACHA NIMREJESHE DARASANI; MWIGULU NCHEMBA

Katika Bajeti 44 trilion zinapigwaje 30 trillion? Alafu na mishahara ya Trilion 20 ikaendelea kulipwa? Huku mtaani miradi ya Matrilion ikaendelea kutekelezwa? Hata hili umeshindwa kuling'amua? 

FIU kwa sehemu kubwa inachambua miamala ya secta binafsi, hicho unachoona kwenye hiyo ripoti yao ni namna Wafanyabiashara wamepata ahueni wanafanya manunuzi makubwa nje ya nchi kwa pesa nyingi wanakuja kuuza kwa faida kubwa, hiyo ndiyo faida ya uchumi wa watu na siyo vitu, awamu yenu mlifunga nchi  biashara zikafa ndio maana hili linakuwa suprise kwenu. Uchumi halisi unapokuwa lazima miamala mingi ifanyike nje na ndani ya nchi kwasababu biashara haina vikwazo wala kufungiwa. Mama karejesha imani ya Wafanyabiashara nchini, wawekezaji wengi wamepata uhakika wa mitaji yao wameamua kuleta mapesa mengi kwa njia ya miamala maana dunia sasa ni cashless economy.

Hakuna mkopo uliovunja sheria, hakuna mkopo ambao haukupitishwa kwenye bajeti. Bajeti ambayo wewe uliiunga mkono kwa kinywa chako binafsi ukatamka "Ndiooo". Kwa taarifa yako tu awamu hii kila kitu kimewekwa wazi wananchi wanaona kila jambo na wanapata muda wa kukosoa, wanajibiwa kwa hoja bila kutekana na kuuana. Awamu yenu mmeliingiza Taifa hili kwenye mikopo umiza (Nyonyadamu) mliyokuwa mnachukua mikopo kimyakimya huku mkidanganya watu kuwa mnajenga kwa pesa za makusanyo ya ndani kumbe ni uongo mkubwa. Tena mlikopa kwa masharti mabovu ya kihuni mkitoa pesa kwa single source kwa makampuni yaliyowapa rushwa na ushahidi upo hadharani CAG kausema. Mlikopa kwenye mabank ya kibiashara yenye riba za kutisha, leo hii unapata wapi uhalali wa kushuku mambo ambayo yako wazi kila mahali?  Mama anatafuta hela kwenye taasisi zenye riba ya chini ya 1%, kila mkopo unawekwa hadharani, unakoelekea panajulikana na kazi inaonekana, hakuna tena blah blah.

SGR inaendelea hakuna kilichosimama, natambua wewe na wenzio hao mnaokesha kupiga majungu mlitarajia mradi huu ukwame ili sukuma gang mjigambe kwamba nyinyi ndio mabingwa na miamba ya nchi hii, hilo mmekwama endeleeni kumeza panadol maana mama hana shughuli ndogo kila kona anapeleka maendeleo. Mama alikuta lot 2 tena zikiwa asilimia za chini sana, kwa muda mfupi kapiga asilimia zaidi ya 90 na kaanzisha nyingine 5, hapa ndio panawafanya mchanganyikiwe kabisa.

Kuhusu uhujumu uchumi, as we speak ulitakiwa uwe gereza la butimba kwa uhalamia na ukatili mkubwa uliowafanyia wavuvi wa nchi hii, umewatia umasikini wa kutisha, ulichoma nyavu zao ukawafunga, wengine wakatoroka nchi, uliwafanyia hivi kwasababu hawakukupa rushwa, hili liko wazi na ushahidi upo.

Nawapa taarifa tu na hao wenzio, nchi imerejea kwenye mstari sahihi, wananchi wana furaha, hawatekwi, hawatishwi, hawabambikiwi kesi, wapinzani wamepewa kila wanachotaka lakini hawana ajenda, uchumi wa watu umeimarika, fedha zinaonekana mtaani, hakuna kilichosimama na miradi mipya ya kutosha.

Mwisho, namba hazidanganyi, ni muda mwafaka urejee darasani, weka tunguli zako likizo, weka ulozi wako pembeni ingia kibwetani, ukitoka huko ndio uje tuzungumzie haya mambo lakini kwa sasa  huna unachokifahamu yamekuzidi kimo.

Post a Comment

0 Comments