Ticker

7/recent/ticker-posts

KAGAME AFUTA SHARITI LA VIZA KWA WAAFRIKA WOTE KUINGIA RWANDA

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefuta sharti la visa kwa Waafrika wote wanaosafiri kuingia Rwanda, na kuifanya nchi yake kuwa taifa la nne barani Afrika kufanya hivyo.

"Kusiwe na makosa juu yake. Mwafrika yeyote anaweza kupanda ndege hadi Rwanda wakati wowote anapotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu,” Rais Kagame alisema.

Aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kufaidisha soko la utalii la Afrika, likisukumwa na ukuaji wa uchumi wa kati barani Afrika.

Rwanda imekuwa kwenye kampeni ya kukuza sekta yake ya utalii, ikishirikiana na vilabu vya soka kama Arsenal na Bayern Munich ili kuitangaza nchi hiyo kama kivutio cha watalii.

Rwanda sasa inaungana na Ushelisheli, Gambia na Benin, kama nchi pekee za Kiafrika zinazotoa viza bila malipo kwa raia wote wa Afrika.

Post a Comment

0 Comments