Ticker

7/recent/ticker-posts

AZIZA ALLY ATEULIWA UBUNGE VITI MAALUM CCM

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa ya NEC imeweka wazi kuwa uteuzi wa Aziza ni kwa mujibu wa Ibara ya 78 (4) ya Katiba pamoja na Kifungu cha 86A (6) na (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343.

Aziza anaziba nafasi iliyoachwa na Bahati Keneth Ndingo aliyejiuzulu nafasi hiyo Agosti 19 mwaka huu na kuwania ubunge wa jimbo la Mbarali, ambako amefanikiwa kushinda.

Post a Comment

0 Comments