Ticker

7/recent/ticker-posts

KUISHI SAYARI YA MARS NI NDOTO YA ELON MUSK ILIYOFELI


Mwaka 2016 Mfanyabiashara tajiri na Mwanaanga nguli Elon Musk alitangaza mpango wa kuunda makao ya binadamu katika sayari Mars na alitaka waliopenda kunufaika na safari hiyo kujiandaa kulipa pesa nyingi ili kufanikisha safiri ya kuelekea katika sayari hiyo. 

Kwa wakati huo safari ya kwenda sayari ya Mars ilikadiriwa kugharimu takribani $.200,000. Musk, aliyekuwa ameanzisha kampuni ya binafsi ya usafiri wa anga za juu ya SpaceX, alitangaza mpango huo katika kongamano la kimataifa la Wataalamu wa anga za juu (IAC) mjini Guadalajara, Mexico. 

Mpango wake, ulijumuisha mfumo wa usafiri ambao ungeweza kusafirisha watu 100 hadi Mars, huko safari yote ikichukua siku 80. 

Na baadaye, safari hiyo ilitarajiwa ichukue siku 30 tu.Musk alitaka binadamu wa kwanza waende Mars mwaka 2022 na alizungumzia mpango wa kuanzisha kizazi cha mwanadam katika sayari hiyo hadi kufikia watu milioni moja na watu hao wangeweza kujitosheleza kwa mambo yote muhimu na akasema mpango huo ungechukua miaka 10 hivi kutimizwa idadi hiyo ya watu 100 wa kwanza.


Kwa maana ingechukua takribani miaka 100 kuwa na watu milioni moja katika sayari hiyo. 

Musk alisema: "Ninataka watu watazame kwamba ni jambo linaloweza kutimia katika zama zetu hizi... na kwamba yeyote anaweza kwenda huko akitaka". "Chini ya mpango huo wa SpaceX, safari ya kwanza ya kumpeleka mwanadamu sayari ya Mars ingefanyika mwaka 2022, japo mpango huo haukufanikiwa hadi kufikia hivi sasa. 

Katika azma yake hiyo Musk alitarajia kukiita chombo chake hicho cha kwanza kupeleka watu sayari ya Mars  kwa jina la "The Heart of Gold," na kingerushwa kutoka Kituo cha Anga za Juu cha NASA cha Keneddy, sehemu muhimu inayotumiwa kurusha roketi na vyombo vya anga za juu Marekani. 

Chombo cha kwanza cha kusafirisha watu kingefanyiwa majaribio katika kipindi cha miaka minne toka taarifa yake hiyo itoke. 

Hata hivyo siku kadhaa baadae Musk alitangaza kwamba majaribio ya kwanza ya roketi ya Raptor yalifanyika kwa ufanisi lengo likiwa kuiweka booster kwenye mzunguko huko anga  za juu.


Musk alisema ukubwa wa Starship kwa ajili ya safari ya Mars ingeweza kubeba hadi abiria 200 na injini ya Raptor ilifanyiwa majaribio Texas na kwamba wakati wa safari hiyo ya siku 80, watu wangeishi kwa pamoja huku wakitazama filamu,  kuhudhuria mihadhara na kucheza michezo isiyoathiriwa wa mvutano wa sayari. Mpango wote huo ungefadhiliwa na Kampuni ya SpaceX. 

Musk aliutazama mpango huo wa kupeleka watu Mars kama "Ushirikiano mkubwa wa umma na sekta kibinafsi" Vyombo vya anga za juu vingetumwa kila baada ya miaka miwili ambapo sayari ya Mars inakuwa imekaribia sana dunia hadi kufikia km. 57.6 milioni.

Kwani wakati mwingine Sayari hizo huwa mbali mno, hadi kufikia km. 400 milioni. Na alidokeza kuwa miaka ya karibuni, umbali huo ulipungua hadi kufikia km. 100 milioni pekee.!

 Lengo kuu la mwanzilishi huyo wa SpaceX pamoja na mambo mengi mengine ilikuwa kumwezesha binadamu kufanya utalii  katika mfumo wetu huu wa Jua

Post a Comment

0 Comments