PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni ugonjwa unaohusisha maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Ugonjwa huo unaweza kuathiri mirija ya fallopian, mfuko wa uzazi, na viungo vya pelvis. Mfumo wa uzazi wa mwanamke ni kama shamba lenye mimea, hupoteza nuru pale inaposhambuliwa na wadudu au ukame. Maambukizi ni kama wadudu waharibifu wanapovamia, wanaweza kuharibu mimea. Hivyo ndivyo maambukizi yanavyoweza kuharibu mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Asilimia kubwa ya Wanawake wamekuwa wakikumbwa na ugonjwa huu huku baadhi yao wamekuwa hawajui dalili wala namna ya kujikinga.
Ugonjwa huu unaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya uzazi na kusababisha matatizo kama ugumba ni salama kwa kila mwanamke kuelewa maana ya ugonjwa huu, sababu zake, matibabu, na hatua za kuchukua ili kuzuia kuambukizwa.
(c) www.woindeshizza.blogspot.com
0 Comments