Ticker

7/recent/ticker-posts

WALIOREKEBISHA MAUMBO YAO WARUHUSIWA KUTOKA MUHIMBILI

WATU wanne waliofanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbo kwa kupunguza uzito wameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila baada ya hali yao kuendelea vizuri ambapo watapunguza kilo 20 hadi 30 kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mtu mmoja aliyefanyiwa upasuaji huo aliruhusiwa kutoka siku ya Oktoba 28 baada ya upasuaji kukamilika na wengine watatu waliruhusiwa kutoka siku ya Oktoba 29, 2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam,Prof Mohammed Janabi leo aliwaambia waandishi wa habari kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza nchini katika Hospitali za Umma na imeandika historia ya kupafanya upasuaji wa kibingwa bobezi wa kupunguza uzito kwa watu wanne wenye uzito uliopitiliza.

Amesema upasuaji huo umefanyika kwa utaalamu wa hali ya juu ambapo wote waliofanyiwa hakuna aliyepasuliwa bali wametumia endoskopia kuingia katika tumbo na kupunguza sehemu ya tumbo la chini na pia kutumia matundu madogo.

Prof. Janabi ameongeza kuwa huduma hii imehusisha wataalamu wa hospitali kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka nchini India, Dk. Mohit Bhandar pamoja na Taasisi ya MedINCREDI.

“Tuliowafanyia huduma hii wana umri wa kati ya miaka 36-40, ambao uzito wao ni kati kilo 107 hadi 142, mmoja aliruhusiwa baada ya masaa nane na wengine watatu waliruhusiwa siku iliyofuata hivyo ukifanyiwa huduma hii haikuzuii kurudi katika majukumu yako kwa wakati” amebainisha Prof. Janabi

Upasuaji huo umetumia saa mbili kukamilika ikiwa ni pamoja kurekebisha  maumbo ya wanawake wanne kwa lengo la kupunguza uzito katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila, jijini Dar es Salaam.



Post a Comment

0 Comments