Ticker

7/recent/ticker-posts

SIMBA YAKIRI MECHI YAO DHIDI YA YANGA NI NGUMU

 Simba imekiri kuwa mchezo wake wa Ligi Kuu utakaochezwa Novemba 5,2023 dhidi ya Yanga ni mgumu.

Akizungumzia mchezo huo Meneja Habari na Mwasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally alisema:Azam hawezi kutufikia tena, mpinzani aliyebaki ni Yanga ambaye na yeye tunataka kumfunga na kumpita kwa alama sita. Ni mechi ambayo tunaitaka kweli kweli, kuanzia kwa mashabiki, benchi la ufundi, wachezaji na viongozi ndio hata hatulali," 

Ahmed Ally ameyasema hayo katika Mkutano wake na wanahabari kuelekea mchezo wao wa ‘Kariakoo Derb'

"Tumewekeza zaidi kwenye kuwafurahisha mashabiki wetu, Jumapili ya Novemba 5, 2023 tunataka kuwafurahisha. Na anayeshinda mchezo huo ndio atatawala nchi hadi tukikutana tena," amesema Ahmed.

"Tumecheza mechi ngumu lakini mechi ya Jumapili ni ngumu kuliko zote hii ni kutokana na utani uliopo pamoja na ubora wa timu yao. Tunaona namna wachezaji wao wanajituma. Mechi yetu dhidi yao ni ngumu kweli kweli, mechi ya kipimo cha mpira wa nchi haiwezi kuwa nyepesi."

Ahmed amewataka mashabiki wa klabu hiyo kijitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa nguvu wachezaji wao, sambamba na hayo amewaasa kuwa watiifu kwa kuzingatia kampeni ya kuhamasisha vitendo vya kiungwana michezoni ‘Fair play’. 

"Mashabiki wetu tuzingatie misingi ya uungwana na ustaarabu, tujitahidi kushangilia na kutaniana kwa heshima ili kuepusha vurugu. Tuendeleze Utanzania kwa utu na upendo." 

Post a Comment

0 Comments