Ticker

7/recent/ticker-posts

UPO UWEZEKANO WA YANGA KUKUTANA NA SIMBA HATUA YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA

TIMU 16 zinazokamilisha hatua ya makundi ya  michuano ya Klabu Bingwa zimashapatikana.

Nchi tatu zimefanikiwa kutoa timu mbili kila moja kwenye hatua hiyo.

Wababe wa soka Afrika, Misri na Tunisia wameendeleza ubabe wa kuwa na zaidi ya timu moja kwenye michuano hiyo, huku Tanzania ikifanya hivyo kwa mara ya kwanza.

Simba na Yanga zimeingia hatua ya makundi. Simba iko kwenye poti la pili na Yanga iko kwenye poti la tatu, zote zikisubiri ratiba ipangwe.

Hii inamaanisha kuna uwezekano Simba na Yanga  zikawa kundi moja kutokana Makundi kupangwa kulingana na kapu nne zinazotokana na alama za timu. 

Katika poti ya kwanza ni lazima utawakuta Al Ahly, Wydad, Esperance na Ma melody

Poti ya Pili watakuwepo Simba, Belouizdad, Pyramid na Petro de Luanda

Poti ya tatu wapo  TP Mazembe, Al Hillal,Asec Mimosas na Yanga 

Huku poti  ya nne wakiwemo Etoile  Sahel,Jwaneng Galaxy FC Nouadhibou na Medeama

Kwenye poti hizi ni kuwa kila poti itatoa timu moja ili kuunda kundi.

Katika kuchagua timu ndipo penye nafasi kubwa ya kuvikutanisha vigogo hivi vya soka Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments