Ticker

7/recent/ticker-posts

JUKWAA LA WAHARIRI LAMPONGEZA MKURUGENZI MPYA WA MAELEZO

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefurahishwa na uteuzi wa Bwa. Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Matinyi ambae awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ameteuliwa Oktoba 1,2023 na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo ambao awali ulikuwa ukishikiliwa na Bwa. Gerson Msigwa ambye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Kwa mujibu wa taarifa ya TEF iliyotolewa leo Oktoba 2,2023 kwa vyombo vya habari ka kusainiwa  na Mwenyekiti wake, Bwa.  Deudatus Balile  jukwaa hilo pamoja na kufurahishwa na uteuzi huo, lakini pia limempongeza Bwa. Matinyi.

" TEF tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uteuzi wa mtu sahihi, kushika wadhifa huo."

Aidha TEF inaamini Matinyi ambae sasa anakuwa na jukumu la kuwa mshauri Mkuu wa masuala ya Habari serikalini, ataifanya kazi yake kwa weledi na ufasa.

Pamoja na mambo mengine TEF inatarajia  kuona Matinyi anakuwa kiunganishi muhimu kati ya  Serikali na vyombo vya Habari nchini.

Aidha TEF  imemkumbusha Matinyi  kuwa hali ya kifedha ya vyombo vya Habari vingi nchini si nzuri hivyo anaweza kuwa kichocheo cha kuishauri serikali kutenga bajeti ya matangazo ili kuvinusuru na anguko la kiuchumi.


Post a Comment

0 Comments