Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ziara yake hivi karibuni nchini Qatar alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi Qatar lililofanyika jijini Doha.
Ameyasema hayo leo tarehe 30 Mei 2023 katika mkutano wake wa kila mwisho wa Mwezi na Waandishi wa Habari uliofanyika Ikulu, Zanzibar.
Dk.Mwinyi amesema alipata fursa ya kueleza maeneo ya uwekezaji na biashara yanayopatikana Zanzibar katika ziara hiyo alipokutana na Wawekezaji Nchini humo.
Aidha Dk.Mwinyi amezungumzia sera ya Uchumi wa Buluu ikiwemo Mafuta na Gesi , Uvuvi, Bandari , usindikaji wa bidhaa za bahari na fursa zinazopatikana katika maeneo ya sekta ya utalii ikiwemo wa fukwe, mambo ya Kale na utalii wa kisasa wa kumbi za Mikutano ya Kimataifa.
Vilevile muda mchache ujao Zanzibar itapokea timu ya wataalamu na Wawekezaji kutoka Qatar.
0 Comments