Ticker

7/recent/ticker-posts

AJIFUNGUA MAPACHA MARA 16, KWA SASA ANA WATOTO ZAIDI YA 30

Mariam Nabatanzi (41) pichani kutoka Nchini Uganda kwa sasa ndie mwanamke anaetajwa kuwa ndio na watoto wengi zaidi Duniani.

Mpaka sasa ameshazaa Watoto 44 na Mwanaume mmoja huku akiwa amefanikiwa kupata mapacha Watatu mara nne, mapacha wanne mara tatu na mapacha wawili mara sita pamoja na mtoto mmoja mmoja mara nane.

Alianza kujifungua watoto hao alipokuwa na umri mdogo, kwa mujibu wa wanasayansi wanasema Mariam ana maumbile yanayomfanya atoe mayai mengi kwa mzunguko mmoja, kati ya watoto wake hao watoto sita wamefariki na kusaliwa na wa watoto 38 ambao wako hai.


Kwa sasa  anawalea mwenyewe watoto wake baada ya mume wake kumkimbia kutokana na kuwa na hali hiyo ya kujifungua watoto wengi kwa uzao mmoja.

Wingi wa watoto na uwezo wa mke wake wa kushika mimba ndani ya muda mfupi baada ya kujifungua, ulimfanya mume wake kukimbia ili kuepukana na gharama za kuihudumia familia yake.

Post a Comment

0 Comments