Na. Pendo Fundisha, Afrinews Swahili-Mbeya
Simanzi imetawala mkoani Mbeya baada ya kutokea kwa kifo cha Mbunge wa Mbarali, Francis Leonard Mtega.
Taarifa ya kifo cha Mtega imethibitishwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson leo Julai 1,2023.
Imebainishwa kuwa Pawatila aina ya Kubota lililokuwa likiendeshwa na Alex Mussa Kibega ndilo lililochukua uhai wa mbunge huyo alasiri ya leo baada ya dereva kushindwa kulimudu na kumgonga mwendesha Mtega ambaye alikuwa akiendesha pikipipiki katika eneo la Kibaoni, tarafa ya Ilongo, Kata ya Chimaya wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea kwenye Barabara ya vumbi ya Chimala Kapunga, ambapo Kibega mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Kibaoni akitokea Kapunga kuelekea Chimala, ilimgonga mbunge huyo mwenye umri wa miaka 59. Mtega alikuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili MC 573CGT aina ya Boxer.
Pamoja na mambo mengine imewekwa wazi kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa opareta wa Pawatila hilo kutochukua tahadhari kwa watumiaji wegine wa barabara. Mtuhumiwa amekamatwa na yuko katika kituo cha Polisi Chimala na mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Wilaya Mbarali.
0 Comments