Ticker

7/recent/ticker-posts

JOKETI:SINA SABABU YA KUMTAJA BABA WA MTOTO

Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, DC Joketi Mwegelo amefunguka jinsi alivyompata mtoto wake, malezi na amewajibu wanaohoji kuhusu ndoa na kumjua baba wa mtoto wake.

Joketi amesema kupata mtoto kwa kipindi hiki haikuwa kwenye mipango yake, alijikuta imetokea na hata ilipotokea akashauliana na baba mtoto wake wakaamua kulea ujauzito, amesema baada ya kupata ujauzito ushauku yake kubwa ilikuwa ni kuona mtoto wake wa kwanza atafananaje, atakuwaje-kuwaje, atakuwa wa kike au wa kiume!!, atakuwa mweusi au mweupe!!. Baada ya mtoto kuzaliwa akawa amefanana zaidi na baba yake huku yeye akimrithisha macho tu.

Ameongeza kuwa suala lingine lililokuwa linampa kigugukizi ni kwenye malezi, namna ya kumlea mtoto kwa mara ya kwanza, lakini anamshukuru Mungu ameweza kumlea vyema ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha kwa wakati hasa kumpa maziwa ya awali ya miezi sita ya mwanzo ambayo ndiyo yenye afya zaidi. Mwegelo amewashauri pia kinamama wanaojifungua wawapatie watoto wao maziwa ya miezi sita ya kwanza kwa kuzingatia afya ya mtoto kwani maziwa hayo ni muhimu sana katika kumkinga mtoto na magonjwa nyemelezi yanayowakumba watoto.

Kuhusu kumuanika baba mtoto na kufunga ndoa, Joketi amesema suala la kumuanika baba mtoto wake kwake halijakaa sawa, hawezi kufanya hivyo na ikiwa wanahabari wanahitaji kumjua basi wafanye upembuzi akinifu wam-baini kisha wamuanike kwenye magazeti na kwenye media mbalimbali lakini wakisibiri kwamba kuna siku atamposti basi watasubiri sana. Pia Joketi amesema vivo hivyo kwa mtoto wake "Toto" kwa sasa hawezi kumuanika mtandaoni hadi hapo atakapoona kuna uhitaji wa kumuanika mtoto wake kwani amekuwa maarufu kwa zaidi ya miaka 15 anawajua walimwengu kwa uchambuzi wa watoto wa mastaa.

Joketi ameongeza kuwa suala la yeye kuolewa siyo jukumu lake kuulizwa, anayepaswa kuulizwa swali hilo ni baba mtoto wake ambaye ndiye mtoaji posa na anayepanga maisha, amesema ni kweli anatamani ndoa lakini yeye hawezi kumuoa mwanaume, mwanaume ndiye anayetakiwa kumuoa mwanamke kwahiyo hata yeye anasubiri maamuzi ya baba mtoto wake kuhusu kumuoa.

Post a Comment

0 Comments