Ticker

7/recent/ticker-posts

MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI YAMEKAMILIKA

Na Eleuteri Mangi, WUSM, Zanzibar

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.  Bi. Tabia Maulid Mwita amesema maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo mwaka huu kitaifa yanafanyika Mjini Zanzibar Julai 7, 2023 yamekamilika na yatakuwa na shamra shamra mbalimbali ikiwemo muziki wa taarab kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Lengo la kuadhimisha Siku ya Kiswahili ni kuieleza dunia kuwa chimbuko la Kiswahili ni Tanzania.

Waziri Tabia amesema hayo Julai 3, mjini Zanzibar wakati wa mkutano wa na waandishi wa Habari mjini humo kutambulisha maadhimisho ya pili ya Siku ya Kiswahili ambayo yalianza kuadhimishwa mwaka 2022 baada ya kutangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema tamasha hilo litahudhuriwa na  watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Ujerumani, Ghana, Kenya, Visiwa vya Comoro na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.


Post a Comment

0 Comments