Ticker

7/recent/ticker-posts

KESI YA MKATABA DP WORLD YAANZA KISIKILIZWA MBEYA

Kesi ya kikatiba namba 5/2023 ya kuhoji uhalali wa mkataba wa uwekezaji wa uendeshaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai imeanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya.

Kesi hiyo imefunguliwa na wadau wa katiba wakiongozwa wakili Boniface Mwabukusi. Wadau wengine waliofungua shauri hilo ni pamoja na Emmanuel Kalikenya Chengula, Alphonce Lusako, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi wakimshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na Katibu wa Bunge. 

Kesi hiyo inasimamiwa na mawikili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi, Philip Mwakilima, Livino Haule na Caroline Luhungu.

Post a Comment

0 Comments