Kijana Ralph Yarl mwenye umri wa miaka 16 ambaye alikua anatafuta wadogo zake ili awarudishe nyumbani amepigwa risasi mbili.
Alikutana na zahama Hilo baada ya kupiga hodi kwenye nyumba ambayo ilikua jirani na nyumbani kwao.
Baada ya kupiga hodi alitokea mzee mmoja ambae alihisi kua Ralph anataka kuiba na ndipo alipofyatua risasi.
na kumpiga kichwani na kumuuliza anatafuta nini?
Kijana Ralph akamwambia anatafuta wadogo zake haikuishia hapo yule mzee aliendelea kufyatua risasi ya pili kichwani.
Kwasasa mjini Kansas hakuna utulivu maandamano na tatizo lililopo ni kuwa kwa Marekani mtu mweusi hapewi thamani sana.
Ralph kwasasa yupo hospital anapambana na hali yake na aliyempiga risasi ni mzungu ambaye yuko uraiani.
Kinachosubiriwa ni kesho polisi wa Kansas city kutatoa taarifa kuhusu suala hilo.
Inasemekana aliyempiga risasi ni mzee wa miaka 84, Mzee huyo alikamatwa na polisi wa Kansas City na aliwekwa rumande kwa saa 24 kisha akaachiliwa.
0 Comments