​
Makamu wa rais nchini Marekani walianza kusafiri kwa ndege kupitia "Air Force Two" mwaka 1959.
Ndege yeyote inayombeba rais aliye madarakani nchini Marekani huitwa "Air Force One" haijalishi ni ndege aina gani.
Jina la "Air Force Two" linarejea kwa ndege yoyote inayombeba makamu wa rais.
Kwa miaka mingi, ndege kadhaa tofauti zimebeba cheo cha "Air Force Two", zikiwasafirisha makamu wa rais na mara kadhaa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Marekani na 'Congress' duniani kote.
Ndege inayotumika sana hivi sasa ni C-32, toleo la kijeshi lililogeuzwa kutoka ndege ya abiria #Boeing757-200.
Makamu wa Rais #Kamala #Harris pia hutumia C-32.
Ndege ya C-32/B757 ni ya kipekee kwa kuwa inaweza kuruka umbali mrefu na kutumia njia fupi za kurukia ambazo si rahisi kwa ndege nyingine kubwa. Boeing iliacha kutengeneza B757 mnamo 2005.
C-32, ina kituo cha mawasiliano, chumba cha mkutano, na viti 32 vya waandishi wa habari/maafisa.
Eneo la mbele lina kituo cha mawasiliano, gali, maliwato na viti 10 vya daraja la biashara.
Sehemu ya pili ni chumba cha kulala maalum kwa matumizi ya makamu wa rais, eneo la kubadilisha, maliwato binafsi, mifumo tofauti ya burudani, viti viwili vya daraja la kwanza vinavyozunguka.
Sehemu ya tatu ina kituo cha mkutano na wafanyakazi na viti vinane vya daraja la biashara.
Sehemu ya nyuma ina viti 32, gali, vyoo viwili na kabati.
Ndani kuna Saa ioneshayo saa tofauti kati ya Washington DC na kule aendapo makamo wa rais.
Rais na makamu wa rais hawasafiri pamoja kwa sababu za usalama.
Ndege inayombeba rais wa Marekani kwasasa "Air Force One" hutumia VC-25, ambayo ni Boeing747 maalumu iliyobadilishwa kijeshi.
Pia ipo Boeing747 maarufu E-4B inayojulikana zaidi kama "ndege ya Siku ya Mwisho"/"Doomsday" au "Nightwatch"
E-4B awali iliundwa kubeba Katibu wa Ulinzi na Wakuu, Pamoja wa wakati wa shambulio la nyuklia
kwa sababu inaweza kutuma amri ya kurusha silaha za nyuklia ikiwa angani, kutoka maghala ya makombora na nyambizi.
Ndege zote VC-25, C-32 na E4B zinawezwa kujazwa mafuta zikiwa angani.
Chanzo:
#insider
#AirForceMagazine
0 Comments