Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amewasili Tanzania usiku wa jana na kupokelewa na mwenyeji wake Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Kamala amewasili nchini akitokea Accra Ghana, ambako alianza ziara yake ya siku tisa barani Afrika, ikihusisha mataifa matatu (ikiwemo Tanzania na Zambia).
Leo kiongozi huyo, atakuwa na ziara katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Makamu huyo wa Rais wa Marekani kutua katika ardhi ya Tanzania na anatarajiwa kuwa na ziara ya siku tatu, inayotazamiwa kujikita katika kukuza uhusiano wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili.
0 Comments