Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Taribo West sasa ni miongoni mwa Wachungaji maarufu akihubiri Injili na kuelezea kufanya miujiza.
Taribo amewahi kukipiga katika klabu za Inter Milan, Derby County, AC Milan na Auxerre ndie mwanzilishi na mwasisi wa Kanisa la Shelter In The Storm Miracle Ministries of All Nation la nchini kwao.
Akiwa mchezaji alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuumiliki na kuuchezea mpira kwa kadiri alivyotaka.
Aidha alifahamika zaidi kwa mtindo wake wa kutengeneza nywele.
0 Comments