Ticker

7/recent/ticker-posts

HISTORIA ILIYOFICHWA, WENGI HAWAJUI KAMA DAR ES SALAAM IPO OLD BOMA

AMEANDIKA ABBAS MWALIMU

Alhamisi tarehe 21 Septemba 2023, nilibahatika kutembelea jengo la Old Boma ambapo kuna ofisi za Dar Es Salaam Centre For Architectural Heritage (DARCH). 

DARCH wanahusika na historia ya Dar es Salaam, tangu wakati huo ikijulikana kama Darra Salaam na baadae Mzizima.

Jengo la Old Boma lipo barabara ya Sokoine, mkabala na Chuo cha Mabaharia (DMI), humo ndimo inapopatikana historia ya Dar es Salaam tangu karne ya nane, wakati huo ikikaliwa na makabila ya Wazaramo na Washomvi.

Jengo la Old Boma lililojengwa na Sultan Sayid Majid Bin Said miaka ya 1860, ni kati ya majengo machache yaliyobaki jijini Dar es Salaam baada ya mengi kuvunjwa na kupoteza sehemu kubwa ya urithi wa kihistoria.

Baada ya kujionea historia hiyo iliyoelezwa kwa  njia ya picha nilijiuliza maswali kadhaa kichwani mwangu:

(i) Ni kwa kiasi gani wakazi wa Dar es Salaam wanafahamu uwepo wa historia hiyo?


(ii) Je, wananchi wanatambua kuwa ndani ya jengo hilo la Old Boma ndipo ilipo historia ya Dar es Salaam?

(iii) Ni juhudi gani imefanyika kuwapa taarifa wananchi wa Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla juu ya uwepo wa historia ya Dar es Salaam ndani ya Old Boma?

(iv) Ikiwa Dar es Salaam ilikuwa na majengo mengi ya kale yaliyovunjwa na ambayo leo hii yangeweza kulifanya jiji hilo kuwa la kitalii na kuingiza mapato mengi, je kuna sheria ya kulinda majengo yaliyobaki yasivunjwe?

(v) Ukiacha jengo la Old Boma, ni majengo gani mengine yaliyopo Dar es Salaam ambayo wananchi wanaifahamu historia yake?

Post a Comment

0 Comments