Ticker

7/recent/ticker-posts

ROYAL TOUR YA RAIS SMIA YAMLETA SANJUY DUTT TANZANIA

Mcheza filamu nguli na maarufu duniani kutoka nchini India ametua nchini kufanya utalii baada ya kutazama filamu ya Royal Tour iliyomuhusisha moja kwa moja Rais Samia Suluhu Hassan.

Dutt mbaye ana zaidi ya wafuasi milioni mia mbili katika mitandao  yake,ametua nchini jana  Septemba 18, 2023.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokewa na Mkurugenzi wa Utalii nchini, Dkt. Thereza Mugobi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damasi Mfugale, bwana Dutt amesema ameamua kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini kufuatia Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha hazina ya utajiri wa vivutio vya utalii nchini.

"Naipenda sana Tanzania, naona nifanye Tanzania kuwa nyumba yangu ya pili sasa baada ya kuitazama filamu ya The Royal Tour" amesisitiza Dutt

Aidha, amesema ameamua  kuwa balozi wa kujitolea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mitandao yake kutokana na mapenzi yake kwa Taifa la Tanzania.

Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt Thereza Mugobi amefafanua kuwa Tanzania imefarijika  kupata ugeni wa msanii huyo maarufu duniani kutoka  India eneo ambalo lina idadi kubwa ya watu takribani bilioni 1.4 ambao ni soko la kimkakati la Tanzania.

"Ujio wa Dutt ni faraja kwetu kwa vile tunatambua  itasaidia  kuwa vuta wageni wengi kutoka bara la Asia ambako yeye anawafuasi wengi" ameongeza Dkt. Mugobi

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Damasi Mfugale amesema Serikali itaendelea  kuwakaribisha watu maarufu duniani ili wasaidie kufikia azma ya kufikisha wageni milioni tano ifikapo 2025 na kuliingizia Taifa dola bilioni  Sita za kimarekani.

Post a Comment

0 Comments