Ticker

7/recent/ticker-posts

YAJUE MAAJABU YA PYRAMIDS ZA MISRI

Mojawapo ya pyramid refu zaidi huko Nchini Misri lina urefu wa futi 481 sawa na jengo lenye ghorofa 48.Lina uzito wa tani million 14.5,limechukua eneo la mraba hekari 13 sawa na viwanja 10 vya mpira wa miguu.Inaaminika kua lilianza kujengwa mnamo mwaka 2540BC (Kabla ya Christi) na kumalizika miaka 23 baadae.

Pyramid kubwa zaidi Misri lilitumia matofali (majabali,) 2,300,000 (million mbili na laki tatu) na inakadiriwa kua kila tofali/jabali/jiwe lilikua na uzito wa tani  7, kwenye kilele cha Pyramid hilo jiwe lililotumika kufunika juu kabisa lina uzito wa tani 50 mpaka leo wazungu wanajiuliza ni kina nani walilipandisha jiwe hilo na ilifanyika vipi jiwe la namna hiyo kupandishwa juu urefu wa futi zaidi ya 400 na binadamu jambo ambalo ni gumu kulielewa 

Pande zote tatu za Pyramid zipo sawa na unaambiwa huwezi kuona kivuli cha Pyramidi hata ukae upande gani hii inamaana kuwa hata jua likae upande gani huwezi kuona kivuli cha Pyramid , hesabu zilizotumika kujenga Pyramid hilo ni pasua kichwa hadi Sasa.

Na Mahmud Suleiman

Post a Comment

0 Comments