Baba Mtakatifu Fransisco amemteua Askofu mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa kuwa Kadinali. Mhashamu Protase Rugambwa ni mwandamizi wa kiti cha uaskofu Jimbo kuu Katoliki la Tabora.Hongera sana Mhashamu Rugambwa.
Taarifa ya uteuzi wake imetoka Vatican.
HISTORIA YA UTUMISHI YA KADINALI RUGAMBWA.
Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa Mei 31,1960, katika eneo la Bunena, Bukoba mkoani Kagera. Alikapandishwa daraja takatifu la Upadri mwaka 1990 kutoka kwa Mtakatifu Yohane wa Pili alipotembelea nchini Tanzania, Septemba 2,1990.
Kutokea hapo alikuwa Padri wa Jimbo Katoliki Rulenge - Ngara.
Kuanzia mwaka 2002 hadi 2008 alifanya utume wake kwenye Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu mjini Vatican.
Baba Mtakatifu Benedikto XVI, Januari 18,2008 alimteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma.
Juni 26,2012 aliteuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa ya Kikisionari na wakati huo huo alipandishwa hadhi na kuwa Askofu Mkuu.
Nobemba 9,2017 Baba Mtakatifu Francisko alimteua kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu.
Baada ya kulitumikia Baraza kwa vipindi viwili na muda wake ulipokwisha kwa mujibu wa Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama "Predicate Evangelism".
Juu ya Sekretarieti Kuu (Curia Romana) na huduma yake kwa kanisa na kwa ulimwengu
Kabla ya leo Julai 9,2023 kuteuliwa kuwa Kadinali, Aprili 13,2023 Baba Mtakatifu alimteua kuwa Askofu Mkuu wenye haki ya kurirhi Jimbo Kuu la Tabora.
0 Comments