Ticker

7/recent/ticker-posts

SERIKALI YAFANYA MABORESHO MAKUBWA TOZO KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII

Na Eleuteri Mangi WUSM Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchema amesema marekebisho ya ada mbalimbali za Serikali na tozo za wakala wa Serikali yanayofanywa ni utekelezaji wa Mwongozo Mpango wa Uboreshaji wa huduma mbalimbali za jamii.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Serikali ya Mapato na Matumizi kwa 2023/24  Juni 15, 2023, Waziri Dkt. Mwigulu amesema miongoni mwa Wizara ambazo zimepata mapendekezo hayo ya ada na tozo ni pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

"Ninapendekeza kuanzisha ushuru wa 1.5% kwenye vinyl,

Mini Disc, Compact Disc, DVD na SD Memory. Hivi ni vifaa vinavyoweza kubeba hakimiliki maudhui ya ubunifu. Ushuru unatarajiwa kuimarishwa utekelezaji wa hakimiliki" amesema Dkt. Mwigulu.

Aidha, ametumia fursa hiyo kutambua mchango wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhamasisha vilabu vya michezo nchini kwa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Klabu ya Simba imefanikiwa kuliwakilisha taifa kwenye ligi ya Mabingwa Afrika na kufika hatua ya robo fainali huku Klabu ya Young African ikiweka rekodi ya kihistoria ya kufikia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. 

"Ni bila shaka hivi vilabu vya michezo vimelipa heshima Taifa letu kimataifa. Mafanikio ya Young Africans SC na Simba SC yameinua kiwango cha taifa letu katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF)" amesema Dkt. Mwigulu. 

Ametumia fursa hiyo kuhamasisha vilabu vingine vya mpira kujifunza kutoka Young Africans SC kwa mafanikio waliyoyapata kitaifa katika miaka miwili mfululizo.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wageni na watendaji wa Serikali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Makatibu Wakuu wengine.

Post a Comment

0 Comments