Mlinda mlango wa Kimataifa wa Tanzania, Benno Kakolanya ameziomba mamlaka zinazotoa uraia nchini ziridhie ombi la winga, Bernard Morrison.
Hivi karibuni Morrison amameuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu kupata uraia wa Tanzania kutokana na mapenzi aliyonayo kwa nchi hii.
Morrison alisema hayo wakati akifanya mahojiano na Global TV Online kupitia video iliyowekwa kwenye YouTube yao masaa ambapo alipiga magoti na kuomba msaada huo kwa Rais.
“Mama Samia naomba nipe passport ya Tanzania, naipenda sana Tanzania na hata kama sitocheza hapa lakini patakuwa nyumbani kwasababu naona kuna mapenzi, hii sehemu ni salama kwahiyo nataka kukaa hapa”. Alisema Morrison.
Vilevile amesema kama atakubaliwa kuwa raia wa Tanzania yupo tayari kucheza timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Kakolanya amemuunga mkono Morrison wakati wa mahojiano yake na kituo cha redio cha EFM leo, ambapo aliulizwa swali juu ya ombi hilo la Morrison.
"Morrison ni mchezaji mzuri, kama ameona haja ya kuwa raia wa Tanzania, apewe nafasi, atatusaidia.
"Ninachokijua wachezaji wengi wa kigeni wanaipena Tanzania, Mimi nadhani apewe tu uraia, atatusaidia." Alisema Kakolanya.
0 Comments