Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 21, 2023 amepokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kupitia, kuchambua na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto za wafanyabiashara nchini.
Taarifa hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt. John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI, Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ahmad Chande, Makatibu Wakuu, Makamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanakamati na wataalam kutoka sekta mbalimbali za masuala ya kodi, biashara na uwekezaji.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri Mkuu amesema Kamati hiyo imefanya kazi kubwa na imeleta majibu ambayo yatatatua changamoto za wafanyabiashara nchini na ameahidi kuwa Serikali imepokea taarifa hiyo na itayafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na kamati hiyo.
Kamati hiyo ambayo ilipewa siku 14, imefanya mapitio katika maeneo mbalimbali ya kikodi, bandari, maeneo ya wafanyabiashara kwenye mikoa mbalimbali nchini.
0 Comments