Ticker

7/recent/ticker-posts

MUSEVENI AKUMBANA NA KELELE ZA MAREKANI NA ULAYA

Uamuzi wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kusaini muswada wa sheria dhidi ya mashoga  na wasagaji uliopitishwa na Bunge nchini humo wiki hii ukiwalenga pia wamiliki wa nyumba watakaokodisha kwa watu wa ndoa za jinsia moja umemuingiza kikaangoni mbele ya Marekani na Washirika wake.

Sasa Rais Museven hataweza kuingia Marekani wala Uingereza na uamuzi huo utawahusu wabunge wote waliounga mkono muswada huo pamoja na Spika wa Bunge la nchi hiyo isipokuwa wabunge wawili ambao walipinga.

Sheria hiyo mpya imweka wazi kuwa adhabu kwa watakaovunja sheria kwa kuchapisha vitabu au, kufadhili kazi hiyo, watatozwa faini ya shilingi milioni 100 za Uganda. Wamiliki wa vyumba vya kufanyia ushoga miaka 7 gerezani, wakati wamiliki wa nyumba watakapangisha kwa mashoga na wasagaji watakabiliwa na kifungo cha miezi 12 gerezani.

Yeyote atakayeshawishi mwingine kufanya mapenzi ya jinsia moja, atafungwa miaka 5 jela  na atakayepatikana na makosa ya kusimamia au kubariki ndoa hizo atafungwa miaka 10 gerezani.


Tayri Rais wa Marekani Joe Biden ameishutumu sheria mpya ya Uganda inayopinga mapenzi ya jinsia moja na kusema kuwa inakiuka haki za binadamu, na inahatarisha maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari  Rais Joe Biden amelaani hatua hiyo ya kupitishwa kwa mswaada huo.

"Ninaungana na watu duniani kote wakiwemo watu wengi wa Uganda katika kuitaka sheria hiyo ifutwe mara moja hakuna mtu anayestahili kuishi kwa kuhofia maisha yake wakati wote au kufanyiwa vitendo vya ukatili na ubaguzi. Ni makosa." imeeleza taarifa hiyo ya Biden.

Post a Comment

0 Comments