Kituo cha Televisheni cha NTV Uganda kimemnukuu Mbunge Asuman Basalirwa akisema kuwa Ubalozi wa Marekani nchini humo, umeifuta VISA ya Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among kutokana na kuhusika kwake kwenye muswada wa sheria ya kupinga ushoga.
Mbunge Asuman ambaye ni miongoni mwa waliotoa hoja ya kupinga ushoga nchini humo ambayo tayari Rais Museveni amesaini kuwa sheria, amewaambia Waandishi kuwa Spika Anita ni miongoni mwa waathirika wa kwanza wa uwezekano wa kuwekewa vikwazo huku akizitaka Balozi hizo kuzuia pia visa ya Rais Museveni na Wabunge wote waliounga mkono muswada huo (isipokuwa wabunge wawili waliogoma kuunga mkono muswada wa sheria hiyo)
Asuman amesema hana shida na namna nchi moja itaamua kudili na maswala yake ya kigeni na kama hekima au demokrasia zao haziwataki viongozi hawa wa Uganda nchini mwao ni haki yao na kwamba hataki mtu yeyote azilaumu Marekani na Uingereza kwa kukataa kuwapa VISA viongozi hao “tatizo langu pekee ni kuchagua Mtu mmojammoja, hii sheria imesainiwa na Rais Museveni naomba kuzialika Marekani, Kanada, Uingereza, Umoja wa Ulaya wafute VISA za Rais Museveni na Wabunge wote isipokua wale wawili waliopinga”
Uganda imepinga na kupuuzia vitisho kutoka Marekani na Jumuiya ya Wafadhili kutokea nchi za Magharibi ikiwa ni pamoja na vitisho vya kuondoa ufadhili, hasa katika Sekta ya Afya na Ulinzi wakisema kuwa kama Bunge la Uganda, wamezingatia maslahi ya Raia wa Uganda na wametunga sheria kulinda ustawi wa Familia za Raia wao, kulingana na Kifungu cha 31 cha Katiba ya Jamhuri ya Uganda.
0 Comments