Ticker

7/recent/ticker-posts

MUHIMBILI, MLOGANZILA WANOGESHA MEI MOSI

Muhimbili Upanga na Mloganzila washiriki  Maadhimisho ya Mei mosi

Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) wameungana na wafanyakazi wengine duniani katika kusherehekea Siku ya  Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) ambayo  kimkoa imeadhimishwa  Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuboresha maslahi ya wafanya kazi ili kuchochea ari ya utendaji kazi kwa kila mtumishi.

“Kwa kutambua umuhimu wa wafanyakazi Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwemo ulipaji wa madeni ya wafanyakazi ,upandishaji wa madaraja na ubadilishaji wa muundo wa utumishi kwa kuzingatia mapendekezo yanayotolewa na Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora” amesema Mwanahamisi.


Pamoja na hayo amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu imeendelea kusimamia utekelezaji wa sheria ya kazi ikiwemo kutatua kero za watumishi mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanatekeleza majukumu yao katika mazingira bora sambamba na kutokomeza vitendo vinavyokiuka sheria za kazi.

“Pamoja na hayo hatuwezi kukwepa ukweli ya kwamba zipo changamoto nyingi zinazowakabili wafanyakazi katika sekta ya Umma na sekta binafsi ambazo utatuzi wake unahitaji upatikanaji wa fedha na zingine zinahitaji kubadilishwa sheria, sera, muundo na miongozo mbalimbali ya utumishi ila niwaahidi kuwa kwa yale ambayo yako ndani ya uwezo wetu kama mkoa tutaendelea kushirikiana pamoja  kuyatafutia ufumbuzi” amefafanua 


Kauli mbiu ya maadhimisho ya Mei mosi mwaka huu ni “Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi,Wakati ni Sasa.”


Post a Comment

0 Comments