Ticker

7/recent/ticker-posts

HAYA HAPA MANENO MAZITO YA MWANAFUNZI ALIYEPOTEZA FAMILIA YAKE

"Naitwa Karen ni mwanafunzi wa kidato cha sita Mwika Sekondari School, ni mwanafunzi ambaye nilikuwa na graduate siku ya tarehe 25 mwezi wa 4  na familia yangu au wazazi wangu ndio walioweza kupata ajali njiani wakati wanakuja kwenye mahafali yangu"

"Hiyo siku ya mahafali saa 12 asubuhi nilimpigia mama yangu mzazi, nilipompigia nikamsalimia nikaongea nae vizuri nikamwambia mama naomba uniletee zawadi ukija akaniambia sawa nimekuletea zawadi na ndugu zako pia wamekubebea zawadi nikamwambia sawa lakini mkifika Moshi mjini hakikisheni mnakunywa chai maana huku mtashinda na njaa"

"Cha mwisho alichonijibu aliniambia tu poa, nilivyomaliza nikamtafuta mama yangu mlezi nikamsalimia tu, nilimtumia meseji nikamwambia shikamo mama!! akanijibu marhaba, hakuongea chochote tena, basi mahafali iliendelea sikufanikiwa kumuona mzazi wangu hata mmoja kwenye mahafali nilipatwa na hofu lakini sikuwa na cha kufanya"

"Baada ya mahafali kuisha nilikutana na rafiki yangu Leonard ndio alikuwa kama baba yangu au mama yangu siku hiyo ya mahafali aliweza kukaa na mimi mwanzo wa tafrija hadi mwisho niliweza kusherehekea na wadogo zangu wa form five pamoja na Leonard kama mzazi wangu, baada ya hapo kila kitu kiliisha tulirudi Mabwenini lakini kumbe wenzangu walikuwa wanajua ila walikuwa wakinificha kilichotokea"

"Siku ya kesho ilipofika asubuhi niliambiwa kwamba mama amepiga simu nimeambiwa niende nyumbani amenifanyia part, nikawambia sawa sikuweza kufikiria kitu chochote kibaya, nilipofika nyumbani nikakuta hali halisi ya msiba na ndipo nilipoweza kupewa taarifa kwamba nimepoteza watu wangu wa karibu wanne ambao ni mama yangu mlezi, mdogo wangu anayenifatia, na watoto wa shangazi yangu wawili"

"Aliyeweza kubaki alikuwa ni mjomba-angu pamoja na mama yangu mzazi ambaye wakati nafika alikuwa Hosptali amelazwa ICU lakini kwa bahati mbaya na yeye amefariki, kwanza sikutegemea kama wasingefika na sikuwahi kufikiria kitu kama kile kingeweza kutokea siku ile, niliamka na matumaini na furaha, nikakaa na wenzangu nikifurahia kwamba namimi leo nitajumuika na ndugu zangu"

"Mama mlezi aliniahidi kwamba ataniletea zawadi ya simu na mama mzazi aliniahidi kwamba ataniletea cheni na bibi aliwapatia viatu waniletee shuleni kama zawadi yake lakini vyote viliweza kupotea katika ajali"

"Nimejifunza mengi, nimejifunza kuwa mkakamavu na mvumilivu, haya ni majaribu tu Mungu anayaleta na mimi naamini Mungu hawezi kukupa jaribu kama huliwezi, NALIWEZA, nimepambana mpaka hapa walikufa kwa ajili yangu lakini mimi pia nitaenda kupambana kwa ajili yao, walinionyesha upendo wa dhati lakini na mimi nitapambana kwa ajili yao, ni dhambi kukata tamaa"- Karen.

Post a Comment

0 Comments