Ticker

7/recent/ticker-posts

CHALAMILA- DAR KELELE HAZIEPUKIKI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo huku akiongezeka kuwa Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukwepa kelele wala kukwepa starehe.

Alisema starehe ya bia haiwezi kwenda bila kelele, aliyasema hayo wakati wa  uzinduzi wa Swahili Comedy Show iliyofanyika Swahili Exprience, Coco Beach Dar es salaam, amesema ni kuhakikisha muziki unaopigwa baa hauwi kero kwa wengine.

 “ Mimi kama RC naahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi, lakini zaidi kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo kwasababu maana na tafsiri ya kelele bado ni jambo ambalo ni gumu kidogo, adhana ikipiga asubuhi asiye Muislamu atasema hizo ni kelele"

"Vyombo vya Kanisani vikipigwa kwa nguvu asiye mkristo atasema ni kelele, miziki ya baa ikipigwa mtu ambaye sio mnywa pombe atasema ni kelele, kwahiyo kuna mahali panahitaji busara kuhusu tafsiri sahihi ya kelele ili Muislamu, Mkristo wapate haki zao, mnywa pombe apate haki yake na asiye imani apate haki yake, kikubwa Dar es salaam huwezi kukwepa kilele, huwezi kwepa starehe."

Post a Comment

0 Comments