Timu ya Yanga imeanza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza WA fainali dhidi ya USM Alger kwenye mchezo uliochezwa kwenye wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Kwenye mchezo huo Yanga imekubali kichapo cha bao 2-1.
Licha Yanga kuutawala mchezo huo katika kipindi cha kwanza, waliruhusu bao kupitia kwa mshambuliaji Aymen Mahious dakika ya 32 ya mchezo,bao Hilo liliwapeleka mpumziko USM Alger wakiwa mbele 1-0.
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutengeneza nafasi nyingi kwaajili ya kusawazisha bila mafanikio.
Kocha wa Yanga akalazimika kufanya mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwa kuwaingiza baadhi ya wachezaji wakiwemo Bernard Morisson, Salum Aboubakar, Djuma Shaban na Lomalisa Mutambala ambapowaliweza kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele, goli likitengenezwa na Morisson dakika ya 82.
Baada ya Yanga kupata bao, USM Alger waliweza kuongeza bao dakika mbili baadae kupitia kwa Islam Merili dakika ya 84.
Matokeo hayo yanaiweka Yanga kwenye mazingira magumu ya kunyakua kombe hilo,kwani mchezo wa pili wanakwenda kuucheza nchini Algeria Juni 3,2023.
0 Comments