Ticker

7/recent/ticker-posts

eRITA KUWAONDOLEA KERO WANANCHI

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), inatarajia kuzindua rasmi mfumo wa kidigitali ambao utasaidia kuwaondolea wananchi adha ya kupata huduma.

Akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini walioshiriki Mkutano wa 12 wa kitaaluma ulioandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) 

Baadhi ya Wahariri wakiwa kwenye mkutano wa 12 wa TEF

Afisa Mtendani Mkuu wa RITA, Angela Anatory amesema wameamua kwenda kidigitali ili kuwapa wananchi nafasi ya kupata huduma popote walipo.

Ameyasema hayo leo mkoani Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine Bi. Angela amesema ingawa bado hawajazindua rasmi mfumo huo, lakini wameiona haja ya kuanza kuutambulisha kwa wananchi.

"Bado hatujauzindua huu mfumo,tunatarajia kuuzindua huu hivi karibuni, lakini tumeiona haja ya kuwashirikisha Wahariri ili wafahamu na kutoa taarifa sahihi na  chanya zenye kukuza Imani kwa wananchi juu ya RITA."


 Mtendaji Mkuu wa RITA, Angela Anatory

Aliongeza kuwa eRITA ni maboresho ya kidigitali yanayolenga kumwesesha mwananchi kuomba na kupata huduma kutoa RITA popote alipo.

"Mfumo huu utamfanya mwananchi kupata  huduma kutoka RITA popote alipo, atalazimika kufika ofisini kuchukua cheti tu."


Alisema mfumo huo mbali ya kurahisisha huduma kwa wananchi lakini pia utaisaidia serikali kupata taarifa sahihi na kwa wakati.

Mfumo huo utaondoa kero ya mwananchi kukutana na vishoka ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwasumbua wataka huduma, lakini pia unafungua dirisha moja la kupata huduma za RITA hatua ambayo inasaidia kuokoa muda.


Aidha mfumo huo utasaidia kuondoa wingi wa saini kwenye cheti cha kuzaliwa na badala yake kutakuwa na sahihi ya Afisa Mtendaji Mkuu pekee kama itakavyokuwa kwenye leseni ya ndoa.

Bi. Angela aliongeza kuwa RITA wanatoa huduma 34 na kati ya hizo, huduma 12 muhimu zikiwemo za vizazi na vifo zimeshaoandishwa kwenye mfumo wa kidigitali.

Post a Comment

0 Comments