INASTAAJABISHA! Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Hanihani, Paul Msabila ameshindwa kuyajua matumizi sahihi ya simu yake ya mkononi na badala yake amejikuta ikimuingiza matatani.
Msabila ambaye anafundisha kwenye shule hiyo ya Hanihani iliyopo kata ya Igunga mjini, amejikuta akipandishwa kizimbani kwa madai ya kutoa vitisho kwa njia ya sim una aliyemtishia ni bosi wake.
Katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Wilaya ya Igunga, Rammy Magoha alidai mbele ya hakimu wa Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 11 mwaka huu saa nne asubuhi katika Kata ya Igunga wilayani humo katika Mkoa wa Tabora.

0 Comments